EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Sunday, September 23, 2012

VURUGU KANISANI: ASKOFU MOKIWA ANUSURIKA KIPIGO KUTOKA KWA WAUMINI, AOKOLEWA NA POLISI

ASKOFU  Mkuu wa Kanisa la Anglikana Tanzania  la  Dk. Valentino  Mkowa leo amejikuta kwenye wakati mgumu baada ya kunusurika kupata kipigo kutoka kwa waumini wake waliokuwa wenye hasira kali.
Askofu Mkuu wa Angikana Tanzania,la Dk. Valentino  Mkowa aliyevuliwa kofia ya kiaskofu akiwa chini ya ulinzi wa polisi waliokuwa wamevalia kiraia wakimtoa nje ya Kanisa la Anglikana la watakatifu wote mjini Sumbawanga baada ya kuzuka kwa vuguru kubwa jana. Picha na Mussa Mwangoka.
Mmoja wa waumini wa kanisa la Anglikana la watakatifu wote la mjini Sumbawanga akiwa na jazba wakati wa vurugu zilizoibuka jana mara baada ya kutolewa uamuzi wa nyumba ya maaskofu wa kuridhia  askofu Mathayo Kasagara kuwa kiongozi wao ambapo vurugu kubwa zilizuka na kusababisha askofu Mkuu wa kanisa hilo Dk Mokiwa kuondolewa akiwa chini ya ulizi wa polisi. picha na Mussa Mwangoka
 Waumini wa Kanisa la Anglikana la watakatifu wote mjini Sumbawanga jana wakipiga kelele kupinga uamuzi wa nyumba ya maaskofu wa kuridhia  askofu Mathayo Kasagara kuwa kiongozi wao ambapo vurugu kubwa zilizuka na kusababisha askofu Mkuu wa kanisa hilo Dk Mokiwa kuondolewa akiwa chini ya ulizi wa polisi. PIcha na Mussa Mwangoka
-------------------------------------------
           Mussa Mwangoka, Sumbawanga-Rukwa Yetu
Vurugu kubwa ziliibuka mara  baada ya kusomwa kwa  tamko lililothibitisha kuwa nyumba ya maaskofu inamtambua  Askofu Canon Kasagara kuwa ni kiongozi wao halali wa kanisa la Anglikana la watakatifu wote Jimbo  la Ziwa Rukwa mjini Sumbawanga.Katibu mkuu wa Anglikana Dk, Dickson Chilongani ndiye aliyesoma tamko hilo mara baada ya kumalizika kwa ibada iliyoongozwa na Askofu Mkuu Dk. Mokiwa.


Akisoma tamko hilo Katibu Mkuu alisema kuwa sehemu ya hoja za msingi kamati ya usimamizi wa kanisa hilo zilidai kuwa uchaguzi uliomweka madarakani Askofu Kasagara uligubikwa na rushwa,si za kweli na  nyumba ya maaskofu imeshindwa kuthibitisha hilo hivyo Kasagara ni askofu wao halali.Kutokana na kauli hiyo waumini hao, walianza kupiga kelele ya kupinga maelezo hayo hali iliyosababisha mjumbe  wa Kamati ya kusimamia kanisa hilo Flugence Lusunzu aliposhika kinasa sauti na kueleza kuwa wanao ushahidi wa kutosha kuwa rushwa ilitumika kwenye kinyang’anyiro cha  uchaguzi huo uliofanyika zaidi ya miaka miwili iliyopita.Alidai kuwa uamuzi wa nyumba ya maaskofu haukuwapa fursa ya kusikiliza upande wa walalamikaji ili hali ushahidi upo wazi, kutokana kauli hiyo zilianza fujo zilisababisha askofu Mokiwa kutolewa lugha chafu, kuvuliwa kufia yake ya kiaskofu, huku wengine warusha viti ambavyo alivikwepa hado alipoondolewa akiwa chini ya polisi waliokuwa wamevalia kiraia.


Hali hiyo iliharibu amani iliyokuwa imetawala ndani ya Kanisa hilo ambapo uligeuka kuwa uwanja wa vita huku waumini wakisikika wakidai kuwa ni heri kanisa hilo lifungwe kuliko Askofu Kasagara kuliongoza.Awali tangu nyakati za asubuhi, polisi waliovaa kiraia walitanda katika viunga vya kanisa hilo ambapo Askofu Mokiwa aliwasili na kulakiwa vizuri na waumini wake waliokuwa wakishangilia kwa nyimbo na mapambio.


Hata hivyo tayari waumini wa Kanisa hilo walionya kwamba askofu Kasagara asikanyage kwenye eneo hilo, kwani kufanya hivyo kunge hatarisha amani onyo ambalo upande wa askofu Kasagara walitii hivyo askofu huyo mwenye makazi yake wilayani Mpanda alibaki katika nyumba moja ya kulala wageni alikokuwa amefikia.Mmoja wa waumini  Julius Michael alisema kwa kuwa waumini wa Jimbo la Rukwa hawamtaki askofu Kasagara hakuna sababu ya kuwalazimishwa lakini  nyumba ya maaskofu inapaswa kuangalia uwezekano wa kuligawa jimbo hilo.


Tayari Serikali imegawa mkoa wa Rukwa na kuzaa ule wa Katavi sasa hakuna umuhimu wa kuwalazimisha waumini wampokee mtu wasiyemtaka nyumba ya maaskofu waanzishe jimbo katika mkoa huo mpya na aongoze Kasagara.Alisema iwapo watatumia nguvu kumuweka Askofu huyo Rukwa haitasaidia kitu kwani hawezi kuwaongoza watu wasiotaka kushirikiana nae.


Mgogoro katika Kanisa hilo umedumu kwa zaidi ya miaka miwili sasa ambapo siku za nyuma waumini hao  walimzuia  Askofu  Mkuu,  Dk  Valentino  Mkowa  kumsimika  Askofu  huyo  na  badala  yake  alisikimkwa  tarehe 16, Juni mwaka jana   Mjini  Mpanda.Kutokana na kujitokeza kwa mgogoro huo, ilifunguliwa  kesi mahakamani ya Hakimu Mkazi Sumbawanga na waumini wa anglikana, Fulgence Rusunzu na Rojas Bendera  na wenzao 191 yenye  namba 11/2011 wakipinga kuchaguliwa kwa askofu Kasagala kuwa kiongozi wa Dayosisi hiyo.Ambayo iliondolewa baada ya pande mbili zinazovutana kukubaliana kuwa baraza la maaskofu ndilo lenye dhamana ya kutatua mgogoro huo.

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate