Meli moja ya abiria kutoka nchini Argentina inazuiliwa nchini Ghana kutokana na nchi hiyo kushindwa kulipa madeni inayodaiwa na wawekezaji wake waliopoteza fedha zao mnamo mwaka 2001 .Meli hiyo iliyokuwa ziarani Afrika, ilizuiwa kuondoka nchini Ghana kufuatia agizo la mahakama.
Kwa upande wake serikali ya Argentina kupitia kwa waziri wake wa mambo ya nje imeshtumu vikali hatua ya kuzuiliwa kwa meli hiyo na kudai kuwa ni njama ya watu wanaotaka kufaidi kiharamu na hivyo kukiuka sheria za kimataifa.Tayari Argentina imezungumza na taifa hilo ili kubadili hatua hiyo ambayo imechangiwa pakubwa na mzozo kati ya Argentina na wawekezaji wake.Ombi hili lilifikishwa mahakamani na kampuni moja yenye makao yake Uingereza ijulikanayo kama NML CAPITAL.
Argentina ndiyo nchi ambayo ilikosa kulipa deni kubwa zaidi duniani, dola bilioni miamoja kati ya mwaka 2001-2002. Hata hivyo madeni hayo yalilipwa huku waekezaji wakipata takriban asilimia thelathini na pesa zao zilizopotea.
via BBC Swahili
No comments:
Post a Comment