EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Thursday, October 4, 2012

Taarifa ya Waziri wa Elimu kwa Umma kuhusu mtihani wa Kidato cha Nne.


Picture

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU MTIHANI WA KIDATO CHA NNE NA MTIHANI WA MAARIFA OKTOBA, 2012

Ndugu Wananchi,
Mtihani wa Kidato cha Nne mwaka 2012 utafanyika nchini kote kuanzia tarehe 08, hadi tarehe 25 Oktoba, 2012. Jumla ya watahiniwa walioandikishwa kufanya mtihani ni 481,414 wakiwemo wavulana 263,202 sawa na asilimia 54.67 na wasichana 218,212 sawa na asilimia 45.33. Idadi hiyo ya watahiniwa wote walioandikishwa mwaka 2012 ni ongezeko la watahiniwa 31,090 sawa na asilimia 6.90 ikilinganishwa na watahiniwa 450,324 walioandikishwa kufanya mtihani huo mwaka 2011. 

  • Watahiniwa wote walioandikishwa kufanya mtihani mwaka 2012 wamegawanyika katika makundi matatu kama ifuatavyo:-
  • Watahiniwa wa shule (School Candidates) ni 412,594 wakiwemo wavulana 228,991 sawa na asilimia 55.50 na wasichana 183,603 sawa na asilimia 44.50.  Watahiniwa hao wa shule wa mwaka 2012 ni ongezeko la watahiniwa 63,204 sawa na asilimia 18.09 ikilinganishwa na watahiniwa wa shule  349,390 wa mwaka 2011.
  • Watahiniwa wa Kujitegemea (Private Candidates) ni 68,820 wakiwemo wanaume 34,211 sawa na asilimia 49.71 na wanawake 34,609 sawa na asilimia 50.29. Watahiniwa wa Kujitegenea walioandikishwa mwaka 2012 ni pungufu ya Watahiniwa 32,114 sawa na upungufu wa asilimia 31.82 ikilinganishwa na watahiniwa 100,934 walioondikishwa mwaka 2011.
  • Mtihani wa Maarifa (Qualifying Test) utafanyika tarehe 16 Oktoba, 2012. Jumla ya watahiniwa wa Mtihani wa Maarifa walioandikishwa ni 21,314 wakiwemo wanaume 8,174 sawa na asilimia 38.35  na wanawake 13,140 sawa na asilimia 61.65. Watahiniwa wa Maarifa walioandikishwa mwaka 2012 ni pungufu ya watahiniwa 8,133 sawa na upungufu wa asilimia 27.62 ikilinganishwa na watahiniwa 29,447 walioandikishwa mwaka 2011. 

Watahiniwa wote wameandikishwa katika shule/vituo vilivyotawanyika katika Mikoa mbalimbali nchini kama ifuatavyo:-  Jumla ya shule 4,155 zina Watahiniwa wa Shule (School Candidates).   Watahiniwa wa Kujitegemea (Private candidates) wameandikishwa katika vituo 902; na Watahiniwa wa Maarifa (Qualifying Test) wameandikishwa katika vituo 616.

Ndugu wananchi,
Hadi sasa maandalizi na usafirishaji wa mitihani hiyo hadi ngazi ya mikoa yamekamilika. Aidha, mikoa inaendelea na taratibu za kuhakikisha kuwa kila kituo kinapata mitihani yake kwa muda uliopangwa kwa kuzingatia taratibu na maelekezo ya Baraza la Mitihani la Tanzania.

Ndugu Wananchi,
Kuhusu usalama wa mitihani, hadi sasa mitihani yote ipo salama, na hakuna mtihani uliyovuja katika ngazi yoyote kuanzia Baraza la Mitihani, Mikoa na Halmashauri. Ninatoa pongezi kwa Baraza la Mitihani kwa kuandaa mitihani hiyo na kuisafirisha kwa usalama hadi ngazi ya mkoa.

Ninatoa wito kwa Kamati za Mitihani za mikoa yote kuhakikisha kuwa taratibu zote za utunzaji, uhifadhi na usafirishaji wa mitihani hiyo zinazingatiwa. Ni matumaini yangu kuwa ufuatiliaji na ukaguzi wa usalama wa kila kituo umefanyika na hatua za kurekebisha mapungufu kama yapo zimefanyika.

Ndugu Wananchi,
Mtihani wa Kidato cha Nne ni muhimu sana kwa wanafunzi na jamii kwa ujumla, kwani hutumika katika uchaguzi wa watahiniwa wanajiounga na masomo ya Kidato cha Tano na Vyuo mbalimbali.  Aidha, ili kuweza kujiunga na soko la ajira katika taasisi za umma au sekta binafsi ni lazima mhusika awe na cheti cha Kidato cha Nne.  Hivyo mtihani wa Kidato cha Nne ni muhimu sana kwa maisha ya watahiniwa na wananchi kwa ujumla.

Ndugu wananchi
Ufanisi wa zoezi muhimu kama la mitihani unahitaji ushirikiano wa wadau wote. Ninatoa wito kwa wananchi wote, wakiwemo Viongozi, walimu, Wazazi, Jamii na  Wasimamizi wa mitihani kutoa ushirikiano wa kutosha na kuhakikisha kuwa mazingira yanakuwa ya amani na utulivu kipindi chote cha mitihani. Wakuu wote wa vituo vya mitihani hakikisheni kuwa mahitaji yote ya msingi kuhusu mitihani yanapatikana.

Ndugu Wananchi,
Kutokana na muhimu wa mtihani wa Kidato cha Nne katika  kutoa mwelekeo wa  maisha ya watahiniwa kama ilivyofafanuliwa hapo juu, wapo baadhi ya watahiniwa na wasimamizi wasio waaminifu ambao wamekuwa wakijihusisha na vitendo vya udanganyifu katika mitihani.  Watahiniwa wanaobainika kufanya udanganyifu katika mitihani wamekuwa wakifutiwa matokeo yao yote ya mitihani kwa mujibu wa Kanuni za Uendeshaji wa Mitihani ya Taifa.

Ninachukua fursa hii kuwakumbusha watahiniwa kuwa, kila mtahiniwa afanye mitihani yake kwa kujitegemea bila udanganyifu. Wale wote watakaobainika kushiriki katika udanganyifu watachukuliwa hatua za kinidhamu. Nikirejea mtihani wa mwaka 2011, jumla ya watahiniwa wa Kidato cha Nne 3,303 walifutiwa matokeo yao kwa sababu ya kufanya udanganyifu. Aidha, walimu waliohusika walipewa adhabu mbalimbali ikiwemo onyo, karipio kali, kuvuliwa madaraka wakuu wa shule na wengine kushitakiwa TSD. Aidha, wenye shule waliothibitika kusababisha udanganyifu wameandikiwa barua ya kusudio la kuzuia kudahili wanafunzi wa Kidato cha Kwanza kwa muda wa mwaka mmoja.

Kuhusu watahiniwa waliofutiwa matokeo, baada ya kuomba msamaha wamepunguziwa adhabu, na wataruhusiwa kufanya mtihani mwaka 2013 kama watahiniwa wa kujitegemea baada ya kutumikia adhabu kwa muda wa miaka miwili. Ninatoa wito kwa walimu, viongozi na wazazi kuwaasa watahiniwa kuhusu swala la udanganyifu, kwani kwa mwaka huu adhabu haitapunguzwa. Ni matumaini yangu kuwa watahiniwa wote watazingatia taratibu zote za mitihani bila kujiingiza katika udanganyifu. Serikali haitasita kuchukua hatua kama ilivyokuwa mwaka 2012.

Ndugu Wananchi,
Ninarudia kutoa wito kuwa walimu, wasimamizi wa mtihani, Wakuu wa Shule, viongozi wote, na jamii kutoa ushirikiano na kuhakikisha kuwa mitihani inafanyika katika mazingira yenye usalama na amani.  Ninaomba wote tuungane kuwaombea Watahiniwa wetu Baraka za Mwenyezi Mungu na mafanikio katika mitihani yao.

Ndugu Wananchi,
Katika kuhitimisha taarifa yangu ninapenda pia kutoa ufafanuzi kuhusu Mtihani wa Taifa wa Kidato cha sita kwa wanafunzi walioko kidato hicho mwaka 2012/2013. Wanafunzi hao watafanya Mtihani wa Taifa mwezi Machi, 2013. Aidha, wanafunzi waliopo kidato cha 3 mwaka huu watafanya Mtihani wa Taifa wa kidato cha 4 mwezi Novemba 2013 kama ilivyoelekezwa na Kamishna wa Elimu kwenye Waraka wa Elimu Na. 5 wa Mwaka 2012 kuhusu Marekebisho ya Mihula ya Shule za Sekondari na Vyuo vya Ualimu.
 
PHILIPO A. MULUGO (Mb.)
NAIBU  WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI

04 Oktoba, 2012


No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate