Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kimepokea fedha kutoka Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HELSB) kwa ajili ya wanafunzi wa mwaka wa kwanza na wanaoendelea na masomo chuoni hapo.Taarifa hiyo ilitolewa na Naibu Makamu Mkuu wa Chuo hicho (Utawala), Profesa Yunus Mgaya, wakati akizungumza chuoni hapo jana.
Naibu Makamu Mkuu wa Chuo hicho (Utawala), Profesa Yunus Mgaya
Alisema fedha za wanafunzi katika chuo hicho walianza kupokea kutoka HESLB tangu juzi na kwamba, kinachoshughulikiwa kwa sasa ni kukamilisha taratibu za hundi za fedha hizo.Profesa Mgaya alisema wanafunzi wa mwaka wa kwanza watawahi kupokea fedha zao endapo watawahi kusajiliwa mapema na kupewa kitambulisho cha chuo na Jumamosi wiki hii wataanza kupokelewa rasmi chuoni hapo.Alithibitisha kuwapo kwa uhaba wa hosteli kwa chuo hicho na kusababisha wanafunzi kulala zaidi ya mmoja kwenye kitanda, ambapo pia alidai ni makosa.Alisema kwa sasa chuo kina zaidi ya wanafunzi 14,000, wakati kina uwezo wa kutoa malazi kwa wanafunzi wasiozidi 6, 849 sawa na asilimia 49 na kwamba, wanafunzi wa mwaka wa kwanza ndio wanaopewa kipaumbele.
alisema fedha hizo hazijafika, lakini HESLB waliahidi wanazituma ndani ya wiki hii.Afisa Habari wa Chuo Kikuu cha Waisilamu, Sudi Mndeme, alisema fedha za malipo ya ada kwa wanafunzi zinapelekwa moja kwa moja katika uongozi wa chuo, lakini za kujikimu wanaingiziwa wanafunzi wenyewe, hivyo hana uhakika kama wameshapewa kwa kuwa chuo hicho kilifunguliwa jana.Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine (Taaluma), Profesa Peter Gilla, alisema mpaka sasa kwao halijawa tatizo kwa kuwa chuo hicho hakijafunguliwa na wanatarajia kufungua Oktoba 15, mwaka huu.Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino (SAUT) cha jijini Mwanza kilisema kinao wanafunzi zaidi ya 1,000, ambao uwapo wao chuoni hapo unategemea upatikanaji wa mikopo kutoka HESLB.
Makamu Mkuu wa SAUT, Dk.Charles Kitima, alisema ingawa chuo hicho kimeshafungua, lakini HESLB iliahidi kupeleka fedha baada ya Oktoba Mosi, mwaka huu.“Ni kweli kwamba, serikali ilielekeza tusifungue vyuo kabla ya Oktoba Mosi, lakini sisi ni chuo binafsi tuna mipango yetu. Ndio sababu tulifungua tangu Septemba 25. Lakini kuhusu mikopo kwa wanafunzi, tuliambiwa tusubiri hadi baada ya Oktoba Mosi,” alisema.Hata hivyo, alisema ni mapema sana kuilaumu HESLB kwamba imechelewesha fedha za mikopo kwa wanafunzi kwa sababu iliahidi kufanya hivyo ndani ya mwezi mmoja baada ya Oktoba Mosi, mwaka huu.
Alisema kimsingi chuo hakiwezi kudai fedha hizo kutoka HESLB, badala yake chuo kitawadai wanafunzi, ambao kama watacheleweshewa fedha hizo ndio watakaoathirika.
“Tuna imani bodi itazingatia ahadi yake ili wanafunzi wasiathirike iwapo watacheleweshewa. Kimsingi wao ndio wanaopaswa kufuatilia sio sisi. Lakini tunaamini mambo yatakwenda vizuri,” alisema.Imeandikwa na Isaya Kisimbilu, Joyce Kakoko, Dar; George Ramadhan, Mwanza na Ashton Balaigwa, Morogoro.
No comments:
Post a Comment