EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Friday, November 30, 2012

Bakwata yamkana Sheikh Ponda mahakamani.

BARAZA Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata), limemkana Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda na wenzake, baada ya kudai mahakamani kuwa eneo walilovamia wakidai ni mali ya Waislamu linamilikiwa kihalali na kampuni ya Agritanza.
 
Katibu Mkuu wa Bakwata, Sheikh Suleiman Lolila alisema hayo jana wakati akitoa ushahidi katika kesi ya jinai inayomkabili Ponda na wenzake 49 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, wakidaiwa pamoja na mambo mengine kuvamia na kupora ardhi na wizi wa vifaa vya ujenzi.Akitoa ushahidi wake jana huku akiongozwa na Wakili Mwandamizi wa Serikali, Tumaini Kweka, Lolila ambaye ni shahidi wa kwanza wa upande wa mashtaka alidai kuwa eneo hilo awali lilikuwa likimilikiwa kihalali na Bakwata.

Hata hivyo, alidai kuwa baadaye Bakwata walibadilishana na Kampuni ya Agritanza Limited baada ya kuona eneo lililobaki halifai kujengwa chuo kikuu kutokana na ufinyu wake.
Alidai kuwa awali eneo hilo lilikuwa kubwa lakini miaka ya 2000 lilianza kumegwa na kuzigawia baadhi ya taasisi na wafanyabiashara na kwamba tume iliundwa na kubaini kwamba hayo yalifanyika kinyume na utaratibu.“Baada ya kumegwa eneo lililobakia ni finyu ambalo halitoshi kujengwa chuo kikuu. Mimi nilikuwapo wakati Baraza la Wadhamini wa Bakwata wakijadili jinsi ya kupata eneo kubwa na kuijadili Kampuni ya Agritanza iliyokuwa na eneo la ekari 40 Kisarawe ili tubadilishane,” alidai.Shahidi huyo aliongeza kuwa Agritanza ilikubali kubadilishana maeneo na kwamba wao walichukua ekari nne zilizopo Markaz (Chang’ombe) na Bakwata ikachukua ekari 40 zilizopo Kisarawe.

“Hayo yalifanyika baada ya kupata baraka kutoka katika Baraza la Maulamaa lililokaa na kuamua hivyo Januari 22, 2011,” alisema shahidi huyo na kuongeza:
“Baada ya kufanyika mabadilishano, Agritanza walianza kushughulikia usajili wa kiwanja namba 311/3/4 na walipata. Hivyo kwa sasa ni wamiliki halali, tulishamalizana nao.”

Shahidi huyo aliendelea kudai kuwa eneo hilo Serikali ililitoa kwa Wamisri kwa ajili ya kujenga chuo chini ya usimamizi wa Bakwata.
Alidai kuwa kwa mujibu wa mkataba huo uliosainiwa mwaka 2003, endapo Wamisri wataondoka Tanzania watarejesha eneo hilo katika umiliki wa Bakwata.
Shahidi huyo pia alitoa kielelezo cha makubaliano ya Baraza la Wadhamini wa Bakwata na Agritanza, kuhusu kubadilishana uwanja.Hata hivyo, Wakili wa utetezi, Juma Nassoro alipinga kwa madai kwamba kisheria walitakiwa kutoa notisi kabla ya kuwasilisha kielelezo hicho mahakamani.Akijibu hoja hizo, Wakili Kweka alidai kuwa barua halisi wanayo na kwamba ipo katika kumbukumbu za Bakwata, huku akisisitiza kuwa shahidi anastahili kutoa kielelezo hicho kwa sababu saini yake ipo.Hakimu Mkazi, Victoria Nongwa anayesikiliza kesi hiyo, alikikataa kielelezo hicho akisema Serikali ilitakiwa kutoa notisi kabla ya kuwasilisha kielelezo hicho.Hakimu Nongwa alisema kwa kuwa barua halisi ipo wanatakiwa kuiwasilisha mahakamani, lakini akasema endapo barua halisi haipo, basi taarifa ya jana itatambulika kuwa notisi na wataruhusiwa.CHANZO CHA HABARI NI MWANANCHI.

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate