WANANCHI wa Kata ya Ketumbeine, wilaya ya
Longido mkoani Arusha wametaka Katiba Mpya itakayoandikwa kuwadhibiti
viongozi na wenye madaraka kutumia nyadhifa zao kujijengea wigo kwa
kuwajaza ndugu,jamaa na marafiki zao kwenye ofisi za umma.
Wakitoa maoni mbele ya Ujumbe wa Tume ya Katiba inayokusanya maonimkoani Arusha, wananchi hao walisema kuna hatari ya ofisi zote za ummakushikiliwa na watoto, ndugu, jamaa na marafiki wa viongozi kutokanana mwanya uliopo kwenye Katiba na sheria zisizowabana viongozi kuhusuajira na uteuzi.
Wakitoa maoni mbele ya Ujumbe wa Tume ya Katiba inayokusanya maonimkoani Arusha, wananchi hao walisema kuna hatari ya ofisi zote za ummakushikiliwa na watoto, ndugu, jamaa na marafiki wa viongozi kutokanana mwanya uliopo kwenye Katiba na sheria zisizowabana viongozi kuhusuajira na uteuzi.
Lemomo Alambala (44), Richard Mollel (28)
na Michael Laizer wote,licha ya kutaka viongozi wadhibitiwe ndugu zao
kwenye medani yauongozi wa ofisi za umma, pia walitaka watakaotuhumiwa
kwa rushwa naufisadi wa mali na fedha za umma kuondolewe madarakani,
kushtakiwa nakufilisiwa wakitiwa hatiani.
“Hatutaki Katiba Mpya iendelee kuruhusu waliokabidhiwa dhamana yauongozi kutumia vibaya ofisi za umma kwa maslahi binafsi. Anayeharibu
kazi asihamishiwe kituo kipya cha kazi, afukuzwe na kufilisiwa,”alisema Laizer
Kuhusu vitendo vya rushwa, Laizer alisema zimetokana na viongozi wengi kupata nyadhifa zao kwa mbinu chafu ikiwamo kuhonga hivyo hutumia ofisi za umma kurejesha fedha walizohonga kwenye uchaguzi.
Alisema rushwa imewafanya viongozi walioingia madarakani kwa njia hiyo kutosikiliza wala kutatua matatizo ya wananchi kwa sababu wana uhakikawa kurejea madarakani uchaguzi utakapoitishwa kwakutegemea nguvu yafedha.
Elizabeth Timotheo (25), yeye alitaka katiba mpya iweke utaratibuutakaowalazimisha wawekezaji wanaotaka kuwekeza kwenye ardhi na rasilimali za Taifa zinazopatikana maeneo ya vijijini kupata kwanza ridhaa ya vijiji husika na halmashauri za wilaya badala ya utaratibu wa sasa.
Via GAZETI LA MWANANCHI
No comments:
Post a Comment