MMILIKI
wa kampuni ya Al Ryami Production, Khalfan Abdallah, ameingia kwenye
lawama nzito kwa kushindwa kwake kuhudhuria mazishi ya msanii Sharo
Milionea yaliyofanyika jana Lusanga wilayani Muheza, Tanga.
Khalfan
ni Bosi wa zamani wa Sharo Milionea, kutokuhudhiria kwake mazishi hayo
kumezua maswali mengi hasa kutokana na ukweli kuwa hakuvutiwa na namna
wasanii wake wa zamani akiwemo Sharo walivyomkiambia.
Wasanii wengine nyota waliotimka kwa Khalfani ni pamoja na Mzee Majuto na Kitale.
Kitale aliiambia Saluti5 kuwa siku ya tukio Khalfan alipigiwa simu na akasema apigiwe baadae ili asikilize kwanza vyombo vya habari kujua kama habari hizo zina ukweli wowote.
Mtu
mwingine wa karibu sana na Khalfan ambaye hakutaka jina lake litajwe,
aliiambia Saluti5 kuwa siku nzima ya juzi (Jumanne) simu zote za Khalfan
zilikuwa zimezimwa, hivyo akaamua kwenda ofisini kwake ambapo huko
akaambiwa Bosi tayari ameenda Tanga msibani.
Mtu
huyo anasema alipofika msibani hakumkuta Khalfan na hata alipowauliza
wasanii wa Bosi huyo wa zamani wa Sharo waliokuwa kambini Tanga mjini
wakawa na majibu tofauti kwamba wanachojua wao ni kwamba Bosi ameenda
Dodoma.
Wasanii
wengi wa vichekesho wameelekeza shutuma nyingi kwa Khalfan na kusema
kwamba hawawezi kumwelewa kwa kitendo hicho cha kutohudhuria mazishi ya
msanii mwenzao.
Saluti5 ilijaribu kumpigia simu Khalfan ili kujua nini kilichomsibu lakini bado simu zake zilikuwa hazipatani.Chanzo cha habari na www.saluti5.com
No comments:
Post a Comment