EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Thursday, November 1, 2012

Dk Nagu azidi kupingwa, UVCCM hali bado tete.


Waandishi Wetu
ALIYEKUWA mgombea wa nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Vijana ya Chama Cha Mapinduzi  (UVCCM),  Agustine Matefu amewasilisha vielelezo kwa viongozi wakuu wa chama hicho, akishinikiza kutenguliwa kwa matokeo ya uchaguzi huo, uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita.
Wakati vielelezo hivyo vikiwasilishwa, wanachama wa CCM, wilayani Hanang’ wamemwandikia  Katibu mkuu wa chama hicho, wakipinga matokeo ya uchaguzi wa kiti cha mjumbe wa Halmashauri  Kuu ya Taifa katika wilaya hiyo yaliyompa ushindi,  Waziri katika Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji na Uwezeshaji),  Dk Mary Nagu.
Matukio hayo mawili yamekuja huku kukiwa na malalamiko mengi kwamba uchaguzi wa CCM na jumuiya zake, ulitawaliwa na vitendo vya rushwa, kitendo kinachowafanya  walioshindwa washinikize kutenguliwa kwa matokeo yote.
Vielelezo vya kuthibitisha namna  uchaguzi wa UVCCM ulivyovurugwa, vimesainiwa na saini za wajumbe 379 wanaopinga matokeo.Vielelezo hivyo ni pamoja na  CD mbili za video zenye sauti zinazoonyesha ukiukwaji wa sheria za uchaguzi baada ya kutawaliwa na rushwa.
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akifungua rasmi mkutano mkuu wa UVCCM, mwishoni mwa wiki  iliyopita, aliwaambia wajumbe kwamba “watajuta” ikiwa watachagua viongozi kwa misingi ya rushwa.“Nawaambieni, mkifanya mchezo ipo siku mtakuja kujuta maana mkishamchagua kiongozi asiyefaa, mtalazimika kuwa naye huyohuyo hadi mwaka 2017 na kama waswahili wanavyosema majuto ni mjukuu,” alisema Rais Kikwete.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Matefu  alisema amewasilisha vielelezo hivyo kwa Rais Kikwete, Katibu Mkuu, Wilson Mkama, UVCCM na Kamati ya Maadili ya CCM.
Matefu ambaye pia ni Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM kutoka katika Mkoa wa Morogoro alisema mwenyekiti wa chama,  anapaswa kutengua matokeo hayo kwa kuwa uchaguzi ulikithiri kwa vitendo vya rushwa.

Alisema katika uchaguzi huo wajumbe waliopiga kura walizidi nusu ya wajumbe wote 700 walioshiriki uchaguzi huo.Alisema jina lake liliondolewa katika mazingira ya kutatanisha na kwamba kitendo hicho kilifanywa na  baadhi ya makada wa UVCCM.“Endapo hakutakuwa na hatua itakayochukuliwa na mwenyekiti, basi sisi tutakwenda katika Mkutano Mkuu wa Chama Taifa (NEC) utakaofanyika Novemba 6 mwaka huu kupinga usifanyike hadi pale hatua itakapochukuliwa,” alisema Matefu.

Matefu alikiri kuwaandaa vijana waliojitokeza wakiwa na mabango ya kupinga ushindi wa mwenyekiti mpya wa UVCCM, wakati  utambulisho wa ugeni huo katika ofisi za makao makuu ya UVCCM.

Sherehe za kuwakaribisha viongozi wapya ziligeuka uwanja wa vita baada ya makundi yanayopingana, kuchapana makonde hadharani na kuwaacha  umati wa watu wakiwashangaa.

Wiki iliyopita, baada ya kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi wa UVCCM mjini Dodoma, kundi la vijana kutoka mikoa mbalimbali walipinga vitendo vya rushwa huku wakiwatuhumu viongozi wa UVCCM na baadhi ya makada wa chama hicho kwa kuhusika.

Waliotajwa ni pamoja na aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa Umoja huo, Beno Malisa, Katibu Mkuu wa UVCCM, Martin Shigela, Hussein Bashe na Fredy Lowassa.

Matefu alisema CD hizo zinawabainisha Bashe, Malisa na Shigela kuwa wahusika wakuu wa vitendo vya rushwa katika uchaguzi huo.

“Malisa na Shigela waligawa Sh1 milioni kwa wajumbe ambao walikuwa wapigakura kitendo ambacho kinakiuka kanuni na sheria za uchaguzi,” alisema Matefu.Hivi karibuni, Bashe alinukuliwa na gazeti hili akikanusha tuhuma hizo akisema si za kweli.“Mimi sijatumwa na Lowassa, wala sifanyi kazi na Lowassa. Nafanya kazi ya CCM, lakini nampenda sana Lowassa kwa sababu ni mmoja wa viongozi na makada wa chama, ambao wameonyesha mapenzi ya dhati kwa CCM na uvumilivu wa hali ya juu,” alisema kada huyo.Katika uchaguzi huo Mbunge wa Donge, Sadifa Juma Khamisi aliibuka mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti wa UVCCM, baada ya kupata kura 483 dhidi ya Rashid Simai Msaraka aliyepata kura 263.

Katika nafasi ya Makamu Mwenyekiti, Mboni Muhita alishinda nafasi hiyo baada ya kupata kura 489 na kumtimulia vumbi mshindani wake, Paul Makonda aliyepata kura 241.Wakati huohuo wanachama wa CCM wilayani Hanang’ wamemwandikia  Katibu mkuu wa chama hicho wakipinga matokeo ya uchaguzi wa mjumbe wa Halmashauri  Kuu ya Taifa wa wilaya hiyo yaliyompa ushindi,  Dk Nagu.Katika barua yao wanachama hao 11 wamesema uchaguzi huo ulitawaliwa na mazingira ya rushwa, kuvunja taratibu za uchaguzi na kwamba matokeo yanapaswa kutenguliwa na uchaguzi kurudiwa.
“Kwa niaba ya wajumbe wenzetu, tunawasilisha kwako pingamizi juu ya uchaguzi uliofanyika Desemba 28 mwaka huu hapa Hanang’ kwa nafasi ya ya Mjumbe wa Halmashauri Kuu Taifa (NEC)” ilisema sehemu ya barua hiyo kwenda kwa Mkama na kuzitaja sababu za kupinga kwao kuwa ni pamoja na kushamiri kwa vitendo vya rushwa vilivyodhihirika tangu hatua ya mwanzo wa uchukuaji fomu mpaka siku ya uchaguzi.
Wanachama hao wamedai kuwa Dk Nagu alikusanya wajumbe pamoja na wanachama wengine na kufanya nao mkutano kwenye eneo la Katesh ambako pia aliwakabidhi matrekta baadhi ya wajumbe wa mkutano mkuu wa  wilaya.Sababu nyingine zilizoorodheshwa na wanachama hao ni pamoja na mshindi huyo kuzunguka katika maeneo na kuwatisha wananchi kuwa kama hatachaguliwa kwenye nafasi hiyo basi wilaya hiyo isitegemee misaada yoyote toka kwake.Kadhalika mgombea alitumia nyadhifa zake kama mbunge na waziri kuwaita wajumbe nyumbani kwake na kufanya nao mikutano ya mara kwa mara.Katika uchaguzi huo, Nagu alikuwa akichuana na Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye ambaye baada ya kushindwa naye alilalamikia vitendo vya rushwa vilivyotawala katika mchakato mzima wa uchaguzi.Imeandikwa na Raymond Kaminyoge na Ibrahim Yamola.”Via Mwananchi.

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate