Mara yangu ya kwanza kuishi Ilala,
Dar es Salaam kwa muda mrefu ni pale nilipokwenda kumtembelea kaka Luka wakati anaumwa miguu kiasi cha
kushindwa kutembea hata hatua moja.
Mbaya zaidi, katika kipindi hichohicho akapata
ugonjwa wa kupooza ‘stroke’, hivyo wazazi wakaniambia nifunge biashara yangu ya
genge, pale Dodoma nije kumsadia
shemeji.
Kaka alikuwa hawezi kwenda chooni,
kwenda bafuni bila kupelekwa na mbaya zaidi kazini kwake, walishamtosa kiaina
kwani misaada ilipungua tofauti na zamani.
“Vipi nyumbani lakini, hajambo baba,
mama?” kaka aliniuliza.
“Kusema ukweli kaka wote wazima, ila
baba naye alikuwa akisumbuliwa na macho, lakini kwa sasa yuko sawasawa.”
“Asante sana kwa taarifa, mimi kama
unavyoniona, ni muda mrefu naumwa, niko ndani tu.”
“Pole sana kaka.”
“Asante mdogo wangu.”
Kwa ujumla maisha pale nyumbani kwa
kaka yalionekana ni bomba. Kwani usafiri mzuri ulikuwepo, nyumba kubwa ya
kisasa, wafanyakazi wawili, mmoja wa shughuli za ndani, mwingine wa kuweka sawa
mazingira kwa ujumla.
Niligundua baada ya kaka kuumwa,
gari alikuwa akiliendesha shemeji.
Jambo moja nilijiuliza moyoni, kama
kaka anaumwa kwa muda mrefu ugonjwa wenyewe ni ule. Je, shemeji anajikidhi wapi
mambo yake ya mapenzi? Maana naye ni binadamu.
***
Wiki moja baada ya kuanza maisha
pale, shemeji alionekana kama kunibadilikia, alionesha dalili zote kwamba
hanipendi na anaombea niondoke maana siku moja aliniuliza kwa macho makavu…
“Hivi shemeji utaondoka lini?”
“Ah! Shemeji, nitaondoka na hali ya
kaka iko hivi..?”
“Kwani wewe daktari?”
“Hata kama siye, lakini siwezi
kuondoka, kwani shemeji nakusumbua kuwepo hapa nyumbani?”
“Mimi sijasema hivyo.”
Nilishindwa kumwelewa shemeji,
lakini pia sikumwambia kaka wala kuwajulisha wazazi kule Dodoma.
Siku moja usiku wa saa sita, alikuja
chumbani kwangu akanigongea mlango, nikajua kaka amezidiwa, nikatoka nikiwa
ndani ya bukta tu…
“Shemeji kuna kitana huku kwako?”
Kabla sijamjibu niliangalia kichwani
kwake, alikuwa na nywele ndefu, tena amezitia dawa, sasa kitana cha nini…
“Sina shemeji, si unajua nywele
zangu hizi, hazihitaji kitana,” nilisema huku nikijishika kichwani kwa
kupapasa.
Aligeuza bila kuendelea na
mazungumzo na mimi, nikarudi chumbani, lakini nilisahau kufunga mlango.
Nilijitupa kitandani nikawa
najiuliza shemeji alitaka kitana cha nini…
“Au kaka kazidiwa sasa anataka
kumpeleka hospitali ndiyo anataka kumchana nywele?”
“Lakini kama ni hivyo, kwanini
asiniite na mimi katika msafara?”
Mara mlango ukagongwa tena…
“Ngo ngo ngo…”
“Karibu,” niliitika kwa sauti ya
chini maana bado nilikuwa niko kwenye mawazo ya ujio wa kwanza.
Safari hii, shemeji alisukuma mlango akaingia ndani. Uso wake ulionesha
ujasiri na ukali, nikahisi amekuja kunifokea kuhusu jambo fulani…
“Hivi kuna kiberiti huku kwako shemeji?”
“Mh! Sijakiona shemeji.”
“Kule mbona hakipo?”
“Wapi, jikoni?”
“Jikoni, kote pia nimekitafuta sijakiona.”
“Dada wa kazi anasemaje?”
“Sijamuuliza, nikajua labda kiko kwako.”
“Huku sidhani shemeji,” nilimjibu huku nikiwa napangua baadhi ya vitu
kukitafuta. Lakini hadi mwishi, kiberiti hakikuonekana.
Shemeji aliondoka bila kuaga nikajua amekasirika sana, nilifunga mlango
kwa funguo, nikarudi kitandani nikiwaza…
“Kesho nimwambie kaka nataka kurudi nyumbani, ni kazi sana kuishi katika
mazingira haya, mtu hampatani sasa tutaishi vipi…
“Nadhani ananitafutia kisa ili anifukuze, ndiyo maana anauliza mambo
mengi, mara kitana, mara kiberiti.”
Sijui ni wakati gani nilipitiwa na usingizi, ila nilikuja kushtuka kwenye
saa kumi alfajiri baada ya kuhisi kitasa cha mlango kinazungushwazungushwa…
“Nani tena saa hizi?” nilijiuliza nikiwa naangalia saa ya kwenye simu.
Nilikwenda kuufungua mlango, shemeji alisimama mlangoni akiwa ndani ya
khanga moja tu, tena aliifunga kwa kukatiza kwenye matiti yake…
“Shikamoo shemeji…”
“Marhaba umeamkaje?”
“Sijambo.”
“Bado umelala?”
“Nilikuwa nimelala, nimeshtuliwa ulivyoshika kitasa.”
“Nilikuwa nataka kukutuma mahali.”
“Sawa shemeji, ngoja nitoke basi.”
Niliruidi chumbani, nikavaa suruali juu ya bukta maana wakati naamka
nilikuwa na bukta tu.
Nilipomaliza kuvaa bukta nilitafuta fulana ambayo ingekuwa rahisi kuivaa
mwilini na kutoka, nikaipata. Wakati natoka, ile nashika mlango tu, nikakumbana
na shemeji naye akiingia, ina maana safari hii alikuwa akiingia bila hodi...
“Karibu shemeji.”
“Asante,” aliitikia kwa sauti ya chini sana...
“Umeshajiandaa?” aliniuliza...
“Ndiyo shemeji.”
“Safari yenyewe nimeiahirisha, pengine mpaka baadaye sana, nitakwambia.”
“Sawa shemeji.”
Nilimwona shemeji akitaka kugeuka ili atoke, lakini kabla hajafanya
hivyo, akaniangalia kwa macho yaliyojaa maswali au wasiwasi...
“Unajua kaka yako anaumwa?” aliniambia.
“Amezidiwa?” nilimuuliza nikiamini hali ni mbaya ndiyo maana alikuwa
akitafuta kitana usiku...
“Kuzidiwaje?”
“Si umeniambia kaka anaumwa sana?”
“Kwani we hujui kama anaumwa?”
“Najua, sasa si umesema anaumwa zaidi?”
“Mimi nimesema anaumwa zaidi au nimekuuliza unajua kama kaka yako
anaumwa?”
“Najua shemeji.”
“Basi ukae ukijua kaka yako anaumwa, mimi ni binadamu kwa hiyo naomba
nichukuliwe kwa ubinadamu wangu ulivyo.”
Sikumuelewa shemeji alikuwa na maana gani kusema vile. Kwani nijuavyo
mimi nilikuja Dar kwake kwa ajili ya kumsaidia kumuuguza kaka Luka...
“Shemeji si ndiyo maana nipo Dar kwa ajili hiyo.”
“Mbona sioni mchango wako.”
“Ah! Shemeji lini nimekataa kukusaidia?”
“Siku zote tangu ulipokuja,” aliniambia, lakini kitu cha ajabu nilimwona
akiachia tabasamu laini huku akiniangalia kwa macho yaliyojaa uchovu.
Nilishindwa kujizuia na mimi nikacheka huku nikimwangalia kwa woga.
Lakini kitu kimoja nilihisi kuna kitu, mazungumzo yake hakuwa akitoa sauti ya
juu. Ilikuwa kama vile hataki watu wajue yuko chumbani kwangu.
“Shemeji nakuja sasa hivi usitoke,” aliniambia akitoka kwa haraka.
Nilikaa kitandani, nikawaza...
“Mh! Hapa pana ishu, tena ishu yenyewe inaweza kuwa ya ajabu.”
Mara mlango ulisukumwa, akarudi tena akiwa tofauti na alivyokuwa mara ya
kwanza...Na IRENE MWAMFUPE NDAUKA.
No comments:
Post a Comment