MUIMBAJI maarufu wa kike hapa nchini, Judith Wambura ‘Lady
Jaydee’ ameanzisha kipindi cha televisheni kitakachorushwa kwa jina la
‘Diary ya Lady Jaydee’ katika kituo cha EATV.
Akizungumza jijini Dar es Salam jana, Jaydee alisema lengo la
kuanzisha kipindi hicho ni kuihabarisha jamii juu ya maisha yake ya
kweli, ikiwa ni kuonesha mambo yote ambayo amepitia katika maisha yake
ya kuielimisha jamii hadi kufikia hapa alipo.
“Haya ndiyo malengo yangu makubwa ili jamii inijue kiundani zaidi,
nilikopitia, nilikotoka mpaka hapa nilipo sasa na ndiyo maana nimeona
kuanzisha kipindi hiki, nina imani jamii itanifahamu ipasavyo,” alisema
Jaydee.
Aidha, Jaydee alitoa shukurani kwa wapenzi wake wa muziki hapa nchini,
ambao humpa sapoti na kuweza kujulikana ndani na nje ya nchi, kutokana
na kazi zake ambazo anazifanya kutambulika ulimwenguni kote.Aliongeza kuwashukuru wanahabari kwa kuwa bega kwa bega na yeye, huku
akiziangukia kampuni kumsapoti ili waweze kutangaza vema soko la muziki
hapa nchini.
No comments:
Post a Comment