ENEO
la machinjio ya ng’ombe na mbuzi, la Vingunguti jijini Dar es Salaam
limeonekana kuzidi kuwa kero na tishio kwa afya kwa wafanyabiashara na
wateja wanaolitumia, kutokana na kukithiri kwa uchafu na harufu mbaya.

Saluti
5 lilizungumza na baadhi ya wafanyabiashara wa muda mrefu katika
machinjio hayo, ambapo walisema kuwa, hali ya kukithiri kwa uchafu na
harufu mbaya inatokana na mpangilio mbovu wa miundombinu.
“Unajua,
jiji linakua na kila uchao na linapokua biashara nayo inapanuka kiasi
cha machinjio haya kuzidiwa,” alisema mmoja wa wafanyabiashara ya nyama
aliyejitambulisha kwa jina la Jumanne Lukwale.
Mfanyabiashara
mwingine aliyetambulika kwa jina la mama Saada alisema kuwa, upo
umuhimu mkubwa wa serikali, kupitia Wizara husika kuyapanua machinjio
haya pamoja na kurekebisha miundo mbinu.
Mama
Saada alisema kuwa, miundo mbinu inayotumika sasa ni ya muda mrefu,
ambako kadri jiji linavyokua, ndivyo nayo inavyozidi kutotosheleza
mahitaji ya watumiaji.Via SALUTI5.
No comments:
Post a Comment