Klabu
ya soka ya Manchester United imepunguza deni lake katika robo ya kwanza
ya mwaka huu, baada ya familia ya Glazer inayomiliki timu hiyo, kulipa
milioni 62.6.
Kwa
jumla, deni lilipungua na kusalia pauni milioni 359.7, katika kipindi
cha miezi mitatu kabla ya tarehe 30 mwezi Septemba, mwaka 2012.

Deni hilo limepungua kwa asilimia 17, ikilinganishwa na mwaka mmoja uliopita.
Mapata
ya Manchester United yalipanda kwa asilimia 3.4, na kufikia faida ya
pauni milioni 76.3, klabu hiyo ya Old Trafford imeelezea.
Lakini
faida kutokana na utangazaji wa mechi zake ilipungua kwa asilimia 37.4,
na kufikia pauni milioni 13.7, hasa kutokana na kubadilishwa kwa ratiba
za mechi.
Klabu
kilicheza mechi moja ya klabu bingwa, ilhali msimu uliopita ilicheza
mechi mbili, na vile vile ilipungukiwa kwa mechi mbili zilizotangazwa
moja kwa moja, ikilinganishwa na msimu wa awali.
Tofauti
hizo zilisababisha hasara ya pauni milioni 5.6, ilhali klabu kina
matumaini kitakuwa katika hali bora zaidi kwa kucheza mechi zaidi za
klabu bingwa.
Manchester
United ilipungukiwa kwa milioni 2.6, kwa kucheza mechi chache za klabu
bingwa, hasa kwa kumaliza katika nafasi ya pili katika ligi kuu ya
Premier, msimu 2011-12, ilikilinganishwa na msimu 2010-11.
Klabu, kwa sasa kinaongoza katika ligi kuu ya Premier.Via www.saluti5.com
No comments:
Post a Comment