WINGU zito limetanda kuhusu nini kinachoendelea kwa mwimbaji wa Twanga Pepeta, Mwinjuma Muumin ndani ya bendi hiyo.
Muumin
hajaoneka kwenye jukwaa la Twanga kwa wiki nzima huku baadhi ya wapenzi
wa bendi hiyo wakianza kuwa na hisia tofauti kuwa pengine mwimbaji huyo
ameachia ngazi.
Saluti5
iliongea na Muumin kwa njia ya simu Jumamosi iliyopita ambapo alisema
ameomba mapumziko mafupi ili akamilishe baadhi ya mambo yake binafsi.(CHANZO CHA HABARI SALUTI5 -www.saluti5.com)

Muumin
maarufu kama Kocha wa Dunia amesema baadhi ya mambo yaliyoko usoni
mwake ni mambo ya kifamilia sambamba na kutengeneza wimbo mmoja wa
taarab.
Muumin
ambaye kwa muda mrefu amekuwa akinukuliwa kuwa ipo siku ataimba taarab
amesema tayari amekamilisha mashairi ya wimbo wake na kazi ya
kutengeneza muziki amemkabidhi Ali Jay “Mwarabu wa Dubai”.
Mapema
mwaka huu Muumin alinukuliwa na luninga ya ITV kupitia kipindi cha Sham
sham za Pwani akisema panapo uhai kabla ya mwaka huu kwisha atakuwa
ametoa wimbo wa taarab na hivyo maandalizi yanayoendelea hivi sasa
yanadhihirisha kutimia kwa kauli yake hiyo.
Hata
Hivyo Muumin alisema hana mpango wa kuachana na Twanga wala kuhamia
kwenye muziki wa taarab bali anataka kuhudhihirishia umma kuwa yeye ni
Kocha wa Dunia kwa kuimba miziki ya aina yote.
Muumin amesema hakuna haja ya kuandikia mate wakati wino upo, watu wajiandae na wategemee changamoto mpya kutoka kwake.
Alisema kabla ya kuamua kustaafu muziki atahakikisha pia anatoa albam ya Bongo Fleva.
Muumin
amesema kwa sasa yupo nyumbani kwao Bagamoyo amepumzika kwaajili ya
matatizo ya kifamilia sambamba pia na maandalizi ya kazi ya taarab.
Saluti5
imepanga kumtembelea Muumin baadae leo huko Bagamoyo ili kujua kwa kina
nini mipango yake ya baadae na pia mapumziko yake yanaisha lini. Stay
tune.
No comments:
Post a Comment