PAMOJA na kukataa kumwanika
hadharani mpenzi wake mpya, staa wa filamu za Kibongo, Jacqueline Wolper
Massawe amesema kuwa akipigwa chini na jamaa yake huyo, atatimka nchi
na kwenda kuolewa ughaibuni.Akiteta na Tollywood Newz hivi karibuni jijini Dar, Wolper alisema
anajitahidi kulilinda penzi lake jipya ili lisiweze kuvunjika na
ikitokea hivyo, hatataka tena kuwa na mpenzi wa Kibongo.
“Kwa kweli
siwezi kuachika tena sasa hivi.Ikitokea sitakuwa na amani moyoni
mwangu na sitataka kuwa na mpenzi mwingine hapa nchini, nitaenda kuolewa
nje ya nchi,” alisema Wolper ambaye hivi karibuni alimwagana na
aliyekuwa mpenzi wake, Abubakar Mtoro ‘Dalas’.Chazo cha hii habari ni Gazeti pendwa la Risasi Mchanyiko uk wa 3.
No comments:
Post a Comment