Kiongozi wa Kanisa wa Katoliki nchini Uingereza
amesema mpango wa serikali ya Uingereza kuhusu ndoa ya wapenzi wa jinsi
moja ni jambo la aibu.
Vincent Nichols
Askofu mkuu wa Jimbo wa Westminster Vincent
Nichols ameiambia BBC kuwa serikali ya Uingereza haina wajibu wa
kuhimiza ndoa ya wapenzi wa jinsia moja nchini Uingereza.
Katika hotuba yake wakati wa ibadi ya Krismasi,
askofu Nichols alisema ndoa kati ya mwanamume na mwanamke inaashiria
mapenzi ya Mungu.
Serikali ya Uinbereza inapanga kuruhusu ndoa ya
wapenzi wa jinsi moja lakini imesema kuwa haitazishurutisha viongozi wa
kidini kuongoza na kuidhinisha ndoa hizo.
Kwingineko, Askofu wa jimbo ya Centerbury
anayeondoka, Rowan Williams amesema heshima na hadhi ya Kanisa la
Kianglikana na nchini Uingereza, limeadhirika pakubwa kutokana na uamuzi
wa hivi majuzi ambao ulipinga uteuzi wa kina mama kama askofu wa kanisa
hilo.Dr Williams anatarajiwa kustaafu kutoka wadhifa huo mwisho wa mwezi huu.
No comments:
Post a Comment