Na Musa Mateja - CHANZO CHA HABARI
www.globalpublishers.info
‘COMEDIAN’ mwenye swaga za kipekee Bongo, Mussa Yusuf Kitale juzikati
alinaswa akifanya shopping ndani ya duka la Robby One Classic lililopo
Kinondoni jijini Dar.

Mpango mzima ulikuwa Desemba 6, mwaka huu ambapo ilibainika kuwa aliteketeza shilingi laki mbili kwa kununua vitu mbalimbali.
Akipiga stori na safu hii, Kitale alisema kuwa siku zote anapenda
kuishi maisha ya kawaida ili kuendana na jamii anayoishi na siku hiyo
aliamua kujihudumia kwa kutumia kiasi hicho kidogo cha fedha.

“Sipendi kuishi maisha ya juu sana maana mimi ni mtoto wa uswazi hivyo
hata shopping zangu mara nyingi zinakuwa za gharama ya chini, ingawa
mara chache huwa nalazimika kutumia fedha nyingi hasa ninapokuwa kwenye
maandalizi ya filamu.”

“Shopping
kama hizi huwa nafanya mara mbili kwa mwezi kwa kuwa tu kazi yangu
huhitaji mavazi tofauti tofauti na ndiyo utakuta nalazimika kufanya
hivyo,” alisema Kitale.




No comments:
Post a Comment