ZAIDI ya familia ya 300 katika Kijiji cha Migoli, Iringa
Vijijini, hazina mahali pa kuishi kufuatia nyumba zao kubomoka na
nyingine kuezuliwa kwa upepo ulioambatana na mvua kubwa.
Mvua hiyo iliyonyesha juzi, ilianza saa 8:00 mchana ikiambatana na upepo mkali uliosambaratisha nyumba 57.
Mvua hiyo iliyonyesha juzi, ilianza saa 8:00 mchana ikiambatana na upepo mkali uliosambaratisha nyumba 57.

Diwani wa kata hiyo, Husein Kiswili. alilithibitisha habari kuhusu tukio hilo na kwamba uharibifu huo umehusisha pia miundombinu ya umeme na barabara katika eneo hilo.
““Hali ni mbaya sana, watu hawana makazi kwa sababu nyumba nyingine zimeanguka, umeme umekatika kwa sababu nguzo zimeangushwa,” alisema Kiswili.
Alisema mbali na nyumba za wananchi pia baadhi ya
vyumba vya madarasa ya shule ya msingi, vimeezuliwa na hivyo
kusababisha wanafunzi kukosa masomo.
Diwani huyo alisema wakazi wa kijiji hicho kwa sasa wanahitaji msaada wa haraka wa kibinadamu.
Mbunge wa Isimani, William Lukuvi, alisema ameagiza timu ya maafa ifanye tathmini kuhusu hasara iliyowakumba wananchi hao, ili aifanyie kazi.
Lukuvi pia aliahidi kutoa mabati kwa ajili ya kuezeka vyumba vya madarasa vilivyoezuliwa na upepo huo.
Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Dk Christine Ishengoma, alitoa kilo 750 zachakula ili kusaidiwa waathirika wa tukio hilo.
Pia aliwataka wananchi kuwa wavuliivu na
kusaidiana katika kipindi hiki kigumu. Dk Ishengoma alisema Serikali
inafanya tathimini ili kujua kiwango cha hasara iliyopatikana kutokana
na mvua hiyo.Via mwananchi
No comments:
Post a Comment