
Mahakama ya ICC yenye makao yake mjini Hague Uholanzi ilitoa uamuzi huo hapo jana na kuamuru kuwa Ngudjolo Chui aachiwe huru mara moja. Kiongozi huyo wa zamani wa wanamgambo huko Kongo DRC alikabiliwa na tuhuma hizo baada ya kuuliwa watu mia mbili katika kijiji cha Bogoro katika mkoa wa Ituri huko mashariki mwa Kongo mwaka 2003. Ngudjolo alikuwa akikabiliwa na makosa saba ya kutenda jinai za kivita na matatu dhidi ya binadamu.
No comments:
Post a Comment