Migogogro ndani ya Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (Chadema), wilayani hapa imeendelea kufukuta
baada ya vijana wadau wa chama hicho kuitisha mkutano wa kuitaka
Halmashauri ya Wilaya ya Karatu kuvirejesha viwanja vya wazi vilivyouzwa
kinyemela na kutishia kuwang'oa viongozi wa halmashauri hiyo.
Halmashauri ya Wilaya ya Karatu tangu mwaka 2000 hadi sasa inaongozwa na Chadema na sasa hivi madiwani wa chama hicho wapo 15 na wa CCM wapo watano.
Vijana hao walitoa maazimio hayo kwenye mkutano wao waliouitisha jana na kuhudhuriwa na wajumbe zaidi ya 75 kujadili hatma ya chama wilayani humo kutokana na kugubikwa na migogoro ambayo imesababisha viongozi kuanza kufukuzana wenyewe kwa wenyewe.
Maazimio mengine waliyoyatoa ni kuwataka viongozi wa juu wa Chadema kuingilia kati kurejeshwa kwa viongozi watatu waliosimamishwa uongozi vinginevyo watatumia nguvu ya umma kuwarejesha kwa nguvu katika ofisi zao ili waendelee na madaraka yao.
Walisema hawana imani na uendeshaji wa ofisi ya Chadema wilayani humo
kwa sababu viongozi waliopo wamekuwa wakitumia muda mwingi kujadili
mambo ya watu badala ya kutafuta mbinu za kukijenga chama ili kiweze
kuimarika kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa 2015.
Halmashauri ya Wilaya ya Karatu tangu mwaka 2000 hadi sasa inaongozwa na Chadema na sasa hivi madiwani wa chama hicho wapo 15 na wa CCM wapo watano.
Vijana hao walitoa maazimio hayo kwenye mkutano wao waliouitisha jana na kuhudhuriwa na wajumbe zaidi ya 75 kujadili hatma ya chama wilayani humo kutokana na kugubikwa na migogoro ambayo imesababisha viongozi kuanza kufukuzana wenyewe kwa wenyewe.
Maazimio mengine waliyoyatoa ni kuwataka viongozi wa juu wa Chadema kuingilia kati kurejeshwa kwa viongozi watatu waliosimamishwa uongozi vinginevyo watatumia nguvu ya umma kuwarejesha kwa nguvu katika ofisi zao ili waendelee na madaraka yao.
Mwenyekiti wa vijana wadau wa Chadema wilaya hiyo, Sadick Sippu, Katibu Lucian Malle na Makamo Mwenyekiti, John Hariohary, wakizungumza na waandishi wa habari jana muda mfupi baada ya kumaliza mkutano huo walisema wameamua kutoa maazimio hayo kwa sababu wamechoshwa na yanayoendelea ndani ya chama.
Walisema viongozi lazima watambue kuwa vijana hawana lengo baya na chama bali wanachotaka ni kuona viongozi waliopo madarakani wanatekeleza majukumu yao kwa kuzingatia katiba ya chama ili kukiwezesha chama kuimarika katika wilaya ya Karatu.
“Wilaya yetu ya Karatu inasifika kuwa kitovu cha upinzani tangu nchi yetu ilipoingia katika mfumo wa vyama vingi vya siasa lakini leo hii kutokana na kuwepo kwa viongozi maslahi ndani ya chama hususani katika wilaya yetu chama kimeanza kwenda mrama,” alisema Sippu.
Hivi haribuni viongozi na wanachama wa Baraza la Vijana la Wilaya ya Karatu (Bavicha) walisema Mbunge wa Karatu Chadema, Mchungaji Israel Natse, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Karatu, Lazaro Masay na Mwenyekiti wa Chadema Wilaya, Thomas Darabe, wajiuzuru nafasi zao ili kurejesha hali ya amani ndani ya chama kwa madai wamekuwa chanzo cha migogoro ndani ya chama.CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment