HATIMAYE
kesi ya msanii nyota wa filamu, Elizebeth Michael “Lulu” imeanza kutoa
mwanga baada ya Mahakama ya Mkazi Kisutu, kuelezwa kuwa upelelezi wa
kesi ya mauaji dhidi ya msanii mwenzake, Steven Kanumba, umekamilika.
Kufuatia
sakata hilo, Lulu sasa atasomewa shtaka la kuua bila kukusudia
(Manslaughter) badala ya kesi ya mauaji ya kudhamiria (Murder) pale
jalada lake litakapofika katika meza ya Mahakama Kuu.
Wakili
wa Serikali, Ofmedy Mtenga alieleza mbele ya Hakimu Mkazi Augustino
Mmbando anayeisikiliza kesi ya msanii huyo aliyeacha gumzo katika
kuhusishwa na kifo cha Kanumba.

“Mheshimiwa
Hakimu, kesi ilikuja kwa ajili ya kutajwa, hivyo upelelezi wake
umekamilika na mshitakiwa alitakiwa kusomewa muhtasari, ingawa Wakili wa
serikali, Tumaini Kweka hayupo,” alisema Mtenga.
Hata
hivyo, Wakili wa mshitakiwa, Peter Kibatala aliiomba mahakama kupanga
tarehe ya karibu ili mshitakiwa asomewe muhtasari wa ushahidi dhidi ya
mashitaka yanayomkabili.
Hakimu Mmbando akikubali kuahirisha kesi hadi Desemba 21
mwaka huu kwa ajili ya mshitakiwa kusomewa muhtasari wa ushahidi na
kisha jalada la kesi litafungwa, kesi itahamia Mahakama Kuu.

Mawakili
wengine wanaomtetea msanii huyo anayetingisha tasnia ya filamu kabla ya
kufikwa na maswahibu hayo ni Kennedy Fungamtama, Peter Kibatala na
Fulgence Masawe.
Msanii
huyo bado yupo rumande kwa miezi nane sasa kutokana na makosa ya mauaji
kutokuwa na dhamana, huku akidaiwa kuwa Aprili 7 mwaka huu alimuua
Kanumba, maeneo ya Vatican, Sinza, jijini Dar es Salaam
No comments:
Post a Comment