Balozi wa Somalia nchini Libya Bwana Abdikani Mohamed
Waeys amesema ana taarifa ya vifo vya raia 18 vilivyotokea kutokana na
ajali ya lori nchini Libya.Wasomali hao wanaotajwa kuwa wahamiaji haramu, 23 wameripotiwa kujeruhiwa huku wengine wakiwa katika hali mbaya.
Wahamiaji haramu wakijaribu kuvuka baharini
Balozi Abdikani amesema lori hilo lililokuwa
limebeba mifuko ya saruji walimokuwa wamejificha Wasomali hao,
lilipinduka na kusababisha vifo, na kusema idadi yao walikuwa 120
wakiwemo wanaume na wanawake wote wakiwa ni Wasomali.Katika miaka ya hivi karibuni idadi ya wahamiaji haramu ambao wamefariki wakijaribu kuvuka baharini imeongezeka.
No comments:
Post a Comment