Binadamu ndivyo walivyo, pale unaposema nampenda sana mwenzangu na ukamwonyesha
mapenzi mazito mazito ndipo atakapokutenda bila kujali maumivu utakayoyapata.
WANAWAKE WANAONGOZA
Tabia hii ipo kwa pande zote mbili, mwanamke na mwanaume lakini kwa undani
zaidi wanawake ndiyo wanaoongoza kwa kumtenda mwanaume aliyeonyesha mapenzi
mazito kwake.
Wengi walioongea na safu hii kwa jinsi zote wanawake ndiyo walizidiwa na skendo
hii ya kutenda wapenzi wao.
Muddy Sukari wa Dar es Salaam yeye anasema aliwahi kumpenda mwanamke kupita
maelezo. Ikafika mahali akaamua kumsomesha hadi chuo kikuu kwa lengo la
kumwongezea elimu ili maisha yawe bora, lakini baada ya kuyapata hayo maisha
bora alimtenda.
MWANAMKE AKIJUA ANAPENDWA HUFANYA HAYA
Kwa mwaname, upembuzi unaonyesha kwamba akishajua mwanaume anampenda sana, huanza maringo, kutotii na kushika njia yake katika mahusiano akiamini hawezi kuachwa kwa sababu anapendwa sana.
Hili linataka kuonyeshwa kwamba, kama mwanaume atampenda sana mwanamke iwe sehemu ya siri ya moyo wake badala ya kumwambia au kumuonesha kwa vitendo.

MWENYE HEKIMA HUFANYA HIVI
Mwanamke mwenye hekima atakapobaini kupendwa sana na mwenza wake ataongeza upendo kwa nafasi yake ili mapenzi yao yazidi kuwa motomoto.
Kila thamani ya ongezeko la penzi kwake kutoka kwa mwenza wake ni deni la kutafuta namna ya kurudisha upendo huo ili kuwe na uwiano.

MWANAMKE ANAYELIPA UPENDO KWA KUMTENDA MWENZA YUKO HIVI
Siku zote mwanamke anayependwa sana lakini yeye akarudisha dharau na kutotii kwa kuamini hawezi kuachwa anatoa majibu kwamba hajampenda huyo mwenza wake ila kuna kitu anachokipata ndiyo maana yuko naye.

NINI CHA KUFANYA KWA WOTE?
Kwa pande zote ni vizuri sana upendo ukalingana katika mizani moja, mwenzio akionyesha anakupenda sana na wewe kazana kuwa mbunifu kutafuta namna ya kujibu upendo wake badala ya kuutumia kumtenda.
Historia inaonyesha kwamba wengi wanaowatenda wenza wao mwisho wao lazima na wenyewe watendwe na kilio chao huwa kikubwa kuliko kilio cha yule aliyemtenda.
Hapo pana kitu cha kujifunza kwamba siku zote mtenda hutendewa na usimfanyie mwenzako jambo ambalo ukifanyiwa wewe huwezi kulipenda hata siku moja.

Tukutane hapa Muda wote ndani ya page yetu ya Mahusiano na Irene Mwamfupe Jamii Blog.
No comments:
Post a Comment