AJALI
mbaya ya gari imetokea usiku huu
tayari maiti 5 zimepatikana huku watu wakijaribu kuwaokoa abiria
wengine.
Basi
la kampuni ya Mtei No. T 827 CDZ limegongana uso kwa uso na Fuso T 765
ACD huku likihusisha pia gari dogo la abiria Hiace No T 203 AQR.
Kwa
mujibu wa ripota wa Saluti5, Adam Kihago ambaye yupo eneo la tukio,
amesema Fuso lilikataa kushika breki kwenye mteremko mkali, likaenda
kuogonga Hiace na kulisukumiza bondeni na kisha Fuso hilo likaenda
kugongana na basi la Mtei uso kwa uso.
Basi
la Mtei lilikuwa linatokea Arusha kuelekea Babati kabla ya kukutana
ajali hiyo eneo la Kiongozi, Kilomita chache kabla ya kufika Babati
mjini.
Kwa hali ilivyo, inaaminika ajali hiyo imesababisha vifo vya watu wengi pamoja na majeruhi wengi.
No comments:
Post a Comment