MWILI
msanii nyota wa filamu, Juma Kilowoko “Sajuki” aliyefariki jana
alfajiri, umeondolewa katika vyumba vya kuhifadhia maiti vya Hospital ya
Taifa, Muhimbili.
Na badala yake, mwili wa Sajuki sasa umekwenda kuhifadhiwa katika chumba cha maiti cha msikiti wa Shadhir (Masjid Shadhully) ulipo kariakoo mtaa wa Sikukuu na Twiga.
Mwili ukiondolewa Hospital ya Muhimbili
Msanii Issa Mussa “Cloud” aliiambia Saluti5 kuwa lengo la kuhamisha mwili huo ni kujaribu kufanikisha taratibu zote za kesho kwenda na muda.
Mwili wa Sajuki ukiingizwa msikiti wa Shadhully
Msikiti wa Shadhully atakaoswaliwa marehemu Sajuki kesho
“Muhimbili process za
kuchukua mwili ni ndefu na hata huduma zao za kuosha mwili wa marehemu
ni ndefu pia kutokana na wingi wa maiti zinahofadhiwa na kuoshwa
hospitalini hapo.
“Hivyo tumeona tuupeleke mwili Masjid Shadhully kwa vile hakuna msongamano kama wa Muhimbili” alisema Cloud.
Masjid
Shadhully ndo msikiti atakaoswaliwa Sajuki hiyo kesho ambapo mwili wake
utachukuliwa msikitini hapo saa 4 asubuhi na kulepekwa nyumbani kwake
Tabata na baadae kurudishwa tena Masji Shadhully kwaajili ya kuswaliwa
na kwenda kuzikwa makaburi ya Kisutu baada ya swala ya Ijumaa saa 7 za
mchana.
CHANZO CHA HABARI NA SALUTI5
No comments:
Post a Comment