Habari zilizotufikia kutoka Jijini Arusha zinaarifu kuwa Askofu wa KKKT Dayosisi ya Kaskazini
Kati, Ask Thomas Laizer amefariki dunia.
Taarifa hizo zinadai kuwa
Ask. Laizer amefikwa na umauti alasiri ya leo katika Hospitali ya Rufaa ya
Selelian ya Mjini Arusha.
Februari 6, 2013 Waziri
Mkuu Mizengo Pinda, alimtembelea na
kumjulia hali Askofu Thomas Laizer wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania
(KKKT) Dayosisi ya Kaskazini Kati.
Taarifa zilipasha kuwa
Askofu Laizer alilazwa Hospitalini hapo kwa zaidi ya mwezi mmoja, na hakuna
daktari wala ndugu aliye tayari kusema ugonjwa unaomsibu.
Pinda alikwenda hospitalini
hapo juzi saa 9 alasiri na kukaa zaidi ya nusu saa, huku waandishi wa habari
wakizuiwa kuingia katika chumba alimolazwa cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi
maalumu.
Hata hivyo, baada ya kutoka
katika chumba hicho kama ilivyo ada ya viongozi kuzungumzia hali ya mgonjwa,
Pinda hakuzungumza na waandishi wa habari na kulikuwa na ulinzi mkali ambapo
pia waandishi wa habari walizuiwa kuzungumza naye.
Awali ilisemekana kuwa Askofu Laizer
amehamishiwa katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC ya Moshi mkoani Kilimanjaro,
baada ya watu wengi kumiminika Selian kutaka kumwona, lakini jana ilidhihirika
kuwa, amelazwa hospitalini hapo.
FK Blog inatoa pole kwa
Waumini na washarika wote wa KKKT nchini kote kufuatia msiba huo mzito
ulilolikumba Kanisa la Kilutheri hasa wakati huu ambao kuna mgongano kati ya
waumini na Viongozi wa Dayosisi ya Kaskazini Kati.
Kwa mujibu wa Radio Upendo FM, baba Askofu Thomas Laizer wa Dayosisi ya Kaskazini katutoka hivi punde.
PICHANI CHINI: Askofu Thomas Leizer, katika siku za mwisho za uhai wake, akiwa chumba cha uangalizi maalum (ICU) katika Hospitali ya Selian Hospital Arusha Centre. Pamoja naye ni Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe. Picha hii ilipigwa Tarehe 3 Februari 2013, ambapo viongozi wa CHADEMA (Mbowe na Lema) walifika kumjulia hali, baada ya kuugua kwa muda mrefu na kulazwa

No comments:
Post a Comment