EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Saturday, February 9, 2013

CHADEMA wamvaa Tendwa kikisema kuwa hakiko tayari kutoa maoni kuhusu vurugu zilizotokea hivi karibuni mjini Dodoma.

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimemwandikia barua kali Msajili wa Vyama vya Siasa, John Tendwa, kikisema kuwa hakiko tayari kutoa maoni kuhusu vurugu zilizotokea hivi karibuni mjini Dodoma.
Sababu kubwa iliyotajwa na chama hicho ni kwamba suala hilo ni la kijinai na msajili hana mamlaka ya kushughulikia makosa ya namna hiyo.

Msimamo huo wa CHADEMA unakuja siku chache baada ya Tendwa kupitia barua yake ya 05/02/2013, yenye Kumb. Na. AB.115/123/01A/45 kumtaka Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk. Willibrod Slaa, atoe maoni yake juu ya vurugu zilizotokea mwishoni mwa juma lililopita.

Katika vurugu hizo wanachama wa CCM, wakiwemo viongozi, wabunge na makada waandamizi, waliwavamia na kuwashushia kipigo wanachama na viongozi wa CHADEMA.

Vurugu hizo zilitokea eneo la Mwanga Bar baada ya wafuasi wa CCM wakiongozwa na mbunge wa Tabora Mjini, Ismail Rage, kung’oa mlingoti na kushusha bendera ya CHADEMA kisha kufanya mkutano wa maadhimisho ya miaka 36 ya kuzaliwa chama hicho.

CHADEMA katika barua hiyo ambayo imesainiwa na Idara ya Sheria ya chama hicho kwa niaba ya katibu mkuu wake, yenye Kumb. Na. C/ADMMSJ/04/04 ya 06/02/2013, wanasema chama hakiwezi kutoa maoni yake, kwa sababu suala hilo ni la kijinai.
Viongozi wake mkoani Dodoma, wameshafungua mashtaka, hivyo kumtaka Tendwa awasiliane na mamlaka zinazohusika na makosa ya jinai.

“Nimeagizwa na katibu mkuu nikujulishe kuwa hatatoa maoni kuhusu tukio lililotokea Dodoma siku ya tarehe Februari 3, 2013 kwa kuwa suala hilo ni la jinai na viongozi wa CHADEMA Mkoa wa Dodoma, wameshafungua mashtaka polisi,” ilisomeka sehemu ya barua hiyo.
Batua hiyo inaongeza kuwa kutokana na suala hilo kuwa la jinai, Msajili wa Vyama vya Siasa hana mamlaka ya kulishughulikia.

Vyama vyaweka mkakati
Kufuatia vurugu zinazoendelea kujitokeza kwenye mjadala ndani ya Bunge kati ya wabunge na kiti cha Spika, vyama vya siasa vyenye uwakilishi bungeni jana vilikutana chini ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, na kuweka mikakati ya kumaliza kasoro hizo.
Katika kikao hicho kilichoitishwa na Mwenyekiti wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD), James Mbatia, viongozi wa vyama hivyo waliziagiza mamlaka husika zitafute mchakato wa kuboresha kanuni za Bunge.

Lengo ni kuongeza ufanisi, uwajibikaji na uhuru katika kazi za Bunge na kuhakikisha kuwa kunakuwa na mfumo imara wa kuendesha Bunge la mfumo wa vyama vingi vya siasa.
Akiwasilisha maazimio hayo ya pamoja, Mbatia alisema viongozi hao waliazimia kuwepo kwa uvumilivu wa kisiasa baina ya vyama vyao na wanachama wake katika kutekeleza majukumu yao katika kudumisha amani, mshikamano na maendeleo endelevu kwa manufaa ya taifa.

Alisema kuwa kuna changamoto mbalimbali kama vile vurugu zilivyotokea bungeni  Februari 2 mwaka huu; kwamba vurugu hizo zinatakiwa kutafutiwa ufumbuzi wa kina ikiwa ni kujenga mahusiano mema, haki, usawa pamoja na kasi ya uwajibikaji ndani na nje ya Bunge.
Viongozi wakuu waliohudhuria mkutano huo, mbali na Pinda ni Makamu Mwenyekiti wa  Chama cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Philip Mangula, Naibu Katibu Mkuu (CCM) Tanzania Bara, Mwigulu Nchemba, Mbataia (NCCR-Mageuzi) na Ambar Haji Khamis, Makamu Mwenyekiti (NCCR Mageuzi).
Wengine ni Augustine Mrema na Jeremiah Sherukindo (TLP), Freeman Mbowe na John Mnyika (CHADEMA), John Cheyo na Izack Cheyo (UDP) na Habib Mnyaa na Julius Mtatiro (CUF) na wawakilishi wa vyama visivyo na wabunge, Fahmi Doutwa na Felix Makuwa (UPDP).

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate