MAMTEI |
MAMTEI amewashutumu wasanii wa tasnia ya filamu
kwa kutojitambua na kuwa watu wanaosemwa vibaya katika jamii na kutokuwa
na makini katika masuala ya msingi.
Wasanii mara nyingi huwa tunajiona kama watoto wadogo, hatuna
nidhamu kabisa. Yaani mahali wanapokusanyika wasanii wengi basi tegemea
vituko au jambo lolote ambalo litamkera mtu mwingine, alisema.
"Hivi ni kwa nini hatubadiliki kila siku ni sisi tu? Lazima tuwe makini katika mambo yanayohusu maisha yetu."
Mamtei alisema hayo kufuatia wasanii wenzake waliokusanyika kwa wingi katika moja ya mikutano iliyoitishwa na shirikisho la filamu kutokea utovu wa nidhamu pale wasanii walipotawanyika katika mkutano huo bila ya kuruhusiwa.
Pia wakati mkutano huo ukiendelea, kulikuwa na minongono mingi jambo lililoashiria wasanii kutofuatilia kilichokuwa kikiendelea mkutanoni.

No comments:
Post a Comment