LOS ANGELES, MAREKANI
CHRIS
BROWN amesema kitendo chake cha kumpiga Rihanna ni kosa baya zaidi
alilowahi kulifanya katika maisha yake, na kuongeza kuwa bado mwanadada
huyo anampenda.
Staa
huyo wa R & B - ambaye bado yupo kwenye kipindi cha uangalizi
kutokana na shambulio alilofanya mwaka 2009 dhidi ya Rihanna anayetamba
na kibao chake ‘Diamonds’, amedai kuwa sasa ni mtu aliyebadilika.
Alisema:
“Wakati mwingine unagombana, unapigana na mtu unayempenda… Usiku ule ni
wa majuto makubwa katika maisha yangu, kosa kubwa. Lakini ananipenda —
ninaweza kusema nini? Mimi ni wa kusamehewa… lakini, ndiyo, ninafanya
kazi kwa bidii kwa ajili ya hilo.”
Wawili
hao ambao walijitenga baada ya tukio hilo, sasa wamerudi tena kuwa
pamoja, na Chris, mwenye umri wa miaka 23, anasisitiza kuwa amejifunza
kutokana na makosa yake na kwamba hataweza kumuumiza tena Rihanna.
No comments:
Post a Comment