![]() |
| Elizabeth Michael ‘Lulu’ |
MSANII nyota wa filamu nchini, Mahfudh Hussein ‘Dk. Cheni’
amebainisha kuwa, hivi sasa wako katika maandalizi ya kucheza filamu na
msanii Elizabeth Michael ‘Lulu’, aliyetoka mahabusu hivi karibuni.
Lulu alikuwa mahabusu tangu Aprili 7 mwaka jana, akikabiliwa na mashtaka ya kuua bila kukusudia, aliyekuwa msanii nguli, Steven Kanumba.
Akizungumza kwa njia ya simu juzi, Cheni
alisema mpango huo umekuja baada ya Lulu kuwa nje ya ulingo wa filamu
kwa zaidi ya miezi saba kutokana na kesi yake inayomkabili.
Alisema hivi sasa Lulu ana kiu ya kucheza filamu, ikiwa ni katika
kudhihirisha kipaji chake, hivyo wamepanga atacheza na kulipwa kiwango
cha juu cha fedha kama mchezaji nyota na siyo mchezaji
aliyeshirikishwa.
“Tutamlipa fedha nyingi Lulu, kwa sababu yeye ni msanii nyota mwenye
mvuto, huku jamii ikiwa na kiu ya kuona kazi zake ambazo hajazifanya
kwa muda sasa,” alisema Cheni.
Alisema kuwa, katika filamu hiyo pia atakuwepo msanii Steve Mengele
‘Steve Nyerere’, ambaye kwa pamoja ndio waliojitokeza kumpa sapoti
Lulu.
Katika hatua nyingine, Dk. Cheni ambaye yuko karibu zaidi na familia
ya akina Lulu, alitanabaisha kuwa, tayari wameshampata mshauri nasaha
kwa kumshauri Lulu ili aweze kurejea katika hali yake ya kawaida baada
ya matatizo yaliyotokea.

No comments:
Post a Comment