SHIRIKA la Umeme Tanzania (TANESCO), limesema kukatika kwa
nishati hiyo katika baadhi ya maeneo ya Kinondoni kunatokana na
matengenzo ya transfoma iliyopo Ubungo jijini Dar es Salaam.
Akizungumza Kamishna Msaidizi wa
Nishati ya Umeme, Innocent Lwoga, alisema kuwa wananchi hawapaswi kuwa
na wasiwasi kwa kuwa hakuna tena tatizo la mgawo wa umeme.
Alisema kukatika kwa umeme katika maeneo hayo kumechangiwa na udogo
wa transfoma hiyo ambayo hivi sasa imezidiwa na wateja, hasa kuanzia
nyakati za saa 12:00 jioni ambapo huduma hiyo hukosekana kutokana na
matumizi makubwa.Lwoga alitaja maeneo ambayo yameathirika ni Kimara, Sinza,
Changanyikeni, Buguruni, Mabibo, Makongo, Salasala na mengine katika
wilaya hiyo.
Alisema shirika hivi sasa linafanya juhudi ya kubadilisha transfoma
hiyo na matengenezo kwa ajili ya kuboresha huduma hiyo, ambapo
yanatarajiwa kukamilika Februari 15.
No comments:
Post a Comment