Ramin Mehmanparast Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran
![]() |
| Ramin Mehmanparast |
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje ya Jamhuri ya Kiislamu
ya Iran amesema kuwa, suala la kufanyika mazungumzo kati ya Iran na
Marekani haliko kwenye ajenda hata ya kiongozi mmoja wa ngazi za juu wa
Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Akizungumza kwenye kongamano
lililohudhuriwa pia na wanafikra wa Kimarekani katika mji wa Mashhad
kaskazini mashariki mwa Iran, Ramin Mehmanparast ameongeza kuwa, kwa
mujibu wa kalibu iliyoainishwa na Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya
Kiislamu, mazungumzo na Marekani hayatafanyika hadi pale Washington
itakapobadilisha nyendo zake za kiadui na viongozi wa nchi hiyo kuiomba
radhi Iran kutokana na siasa zake za chuki dhidi ya taifa la Iran.
Mehmanparast ameongeza kuwa, suala la kufanya mazungumzo na kunyanyua
kiwango cha uhusiano na nchi mbalimbali, ni jambo linalopewa kipaumbele
katika siasa za kigeni za nchi yoyote ile ikiwemo Iran na kusisitiza
kuwa, kabla ya hapo Marekani mara kadhaa imekuwa ikitaka kufanya
mazungumzo na Iran kwa lengo la kutatua migogoro mbalimbali katika eneo
kama vile mgogoro wa Afghanistan.
Mehmanparast amebainisha kuwa,
mazungumzo yanayokwenda sambamba na vitisho, mashinikizo ya kisiasa na
kiuchumi kamwe hayana nia njema na kuongeza kuwa, Washington kamwe
haiwezi kuwadhibiti wananchi wa Iran kwa kutumia vitisho, vikwazo na
mashinikizo. Chanco na Radio Iran.

No comments:
Post a Comment