
Timu ya taifa ya soka ya Burkina Faso jana ilifanikiwa kuingia
fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika baada ya kuinyuka Ghana mabao 3
kwa 2 kwa mikwaju ya penalti. Timu zote mbili za
Burkina Faso na Ghana
zililazimika kupiga mikwaju ya penalti baada ya kutoka sare ya bao moja
kwa moja katika dakika zote za mchezo huo.
Sasa Burkina Faso itachuana na Nigeria katika fainali ya Kombe la
Mataifa ya Afrika. Nigeria imeingia fainali baada ya kuinyuka Mali mabao
4 kwa 1. Mashindano hayo yanafanyika nchini Afrika Kusini.
Katika mechi za kuwania Kmbe la Mataifa ya Asia, timu ya taifa ya
Jamhuri ya Kiislamu ya Iran pia jana iliinyuka timu ya taifa ya Lebanon
mabao matano kwa sifuri. Mechi hiyo ilikuwa ni ya hatua ya kwanza ya
mechi za awali za kuwania tiketi ya kucheza fainali za Kombe ya Mataifa
ya Asia mwaka 2015.
Katika mechi muhimu za kirafiki zilizofanyika jana timu ya taifa ya
Uingereza imeichapa Brazil mabao mawili kwa moja katika uwanja wa
Wembley, Ufaransa imechapwa mabao mawili kwa moja na Ujerumani, Italia
na Uholanzi zimetoka sare ya bao moja kwa moja na Argentina imeikung'uta
Sweden mabao 3 kwa 2.
No comments:
Post a Comment