EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Saturday, February 16, 2013

Maandamano yatikisa, zaidi ya watu 90 wanaswa

SHUGHULI katika Jiji la Dar es Salaam jana zilisimama kwa muda baada ya wafuasi wa Katibu Mkuu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu nchini, Sheikh Issa Ponda, kuandamana huku wakipambana na askari polisi waliotanda katika maeneo mengi ya mji.  
 
Wafuasi hao waliotawanywa mara kwa mara na kwa mabomu ya machozi na askari polisi, walitumia stali mpya kuandamana hadi kwenye Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP), kufikisha ujumbe wao.

Vurugu hizo za polisi kupambana na waandamanaji hao zilianza mchana baada ya swala ya Ijumaa hadi saa 9:00 alasiri huku mitaa mingi katika jiji la Dar es Salaam ikiwa wazi kutokana na watu wengi kuondoka maeneo hayo.
Watu hao waliandamana kushinikiza Ponda ambaye yupo ndanmi akikabiliwa kesi ya wizi na uvunjifu wa amani ashiwe kwa dhamana.


Watu hao walitokea katika misikiti mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam baada ya swala ya Ijumaa ikiwemo, Kwamtoro, Magomeni na Buguruni kuelekea ofisi za DPP zilizopo barabara ya Ohio na Sokoine eneo la posta wakiwa katika vikundi vidogovidogo, tofuati na mandamano ambayo yamezoeleka kufanyika.

Hata hivyo, Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya  Dar es Salaam inawashikilia zaidi ya watu 90 ambao walishiriki kuhamasisha na kufanya maandamano.
Kaimu wa Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Mohamed Msangi alisema kati ya watu hao watawahoji ili kuwabaini wahusika wakuu na kufikishwa mahakamani.
“Kama inavyofahamika wazi kwenye  msafara wa mamba kenge hawakosekani sasa tutawahoji ili tuweze kuwapata wahusika wakuu na tuweze kuwachukulia hatua za kisheria kwani hao ni wavunjifu wa amani,”alisema.

Msangi alisema jeshi hilo lilipiga marufuku maandamano hayo lakini watu hao wamekaidi amri hiyo na kwamba sasa watachukuliwa hatua za kisheria.
Alisema kulikuwa na vikundi vya watu katika maeneo ya Buguruni, Mnazi Mmoja na Kariakoo ambao walikuwa katika makundi huku wengine wakiandamana katika makundi
“Tumeweza kuchukua hatua kwa watu waliyokuwa wanataka kujaribu kuvunja amani kwa kufanya maandamano  kwani tumedhibiti hali hiyo na kuweza kuwakamata watu 80 ambao wapo katika kituo cha Polisi Kati  na Msimbazi,”alisema Msangi.
Alisema hali sasa ni shwali na kwamba vurugu ambazo zilitaka kujitokeza zimedhibitiowa.

Maandamano
Majira ya saa7:45 mchana askari waliyokuwa wameva nguo za kiraia na wengine  walikiwa katika sare za Jeshi la Polisi walitanda  njia zote zinazopita eneo la Ofisi ya Mkurugenzi wa Mshitaka nchini DPP huku wakitoa tahadhari kwa watu waliokusanyika pamoja kutawanyika.
Kadri muda ulivyokuwa ukienda ndipo idadi ya askari ilivyozidi kuongezeka huku wakiwa wameshikilia silaha za moto.

Mbinu wazotumia askari
Askari walikuwa wakitumia pikipiki za mikuu miwili maarufu kama boda boda kuzungukia mitaa ya katikati ya jiji kwa lengo la kuwasambaratisha waandamanaji hao.
Askari wengine walikuwa wakitumia magari ya kiraia kuzunguka katika mitaa ya katikati ya jiji ambapo walipokuta mikusanyiko ya watu walikuwa wakiwakamata na kuwachukua katika magari hayo.
Msikiti wa Mtoro
Katika hali ya kushangaza Imamu wa Msikiti wa Mtoro alisikika akiwatangazia waumini wake kuwa waislam hawatakiwa kuogopa bali wanatakiwa kuandamana kwenda kwa DPP.
 “Ukiwa Muislamu hutakiwi kuogopa kutetea haki yako,siku ya leo maandamano ni lazima,”alisema Kiongozi huyo ambaye jina lake alikupatikana mara moja.
Baada ya tangazo hilo Waislamu hao, walitawanyika na kujigawa mmoja mmoja  kitu ambacho kilionekana kuwachanganya Askari Polisi Kikosi cha kutuliza ghasia (FFU).
Baada ya kufika mbele ya jengo la polisi la Msimbazi watu hao walianza kuungana kwa makundi na kufanya Polosi waliokua kwenye doria kuwazuia kuendelea na safari na walipo kaidi agizo hilo walianza kuwafukuza kwa kutumia mabomu ya machozi.

Msikiti wa Temeke Tungi
WATOTO kuanzia miaka kati ya nane hadi tisa walionekana kwenye lango kuu la kuingilia kwenye msikiti huo wakigawa vipeperushi ambavyo vilikuwa vinawahamasisha waumini hao kuandamana hadi kwa DDP kwa kile kilichodaiwa viongozi wa waislam hawapatiwi dhamana.
Kipeperushi hicho kinasema “Kimsingi mfumokristo ndani ya Serikali unawahujumu waislamu hivyo wanapaswa kuendelea kupambana kukataa kufanywa raia daraja la pili.
IIiendelea kusomeka hivi, “tukumbuke madhalimu hawarudi nyuma kama Shekh Ponda ataendelea kunyimwa haki yake ya dhamana Alhamisi hii,mara baada ya swala ya ijumaa waislamu wote wanatakiwa kuandamana kuelekea kwa DDP,akatueleze kwa nini viongozi wa waislamu hawapati dhamana”

Ilipofika saa 6:20 mawaidha yalianza kwa kuionya serikali kwa kutowadhamini waumini wa dini hiyo kwa kile walichodai kutomtendea haki Sheikh Ponda kwa kutompa dhamana.
Mmoja wa maimamu wa msikiti huo alisema walimwandikia barua DDP ili aweze kukutana nao kujadili suala la kupewa dhamana hiyo lakini akawataka wakutane Februali 28 mwaka huu.

Hali tete Buguruni
Kilionekana kikundi cha dini ya kislamu wakiandamana huku wakiimba Takbir wakielekea  Kariakoo lakini walitawanywa kwa kurushiwa mabomu ya machozi na askali wa jeshi la polisi waliokuwa zaidi ya saba waliojazana kwenye Defender moja.
Baadaye lile kundi liliungana na waislamu kutoka msikiti wa Ilala ambao walitupiwa mabomu  ya machozi zaidi ya manne ili kuwatawanyisha waandamanaji hao na kusababisha  magari kusimama zaidi ya dakika 30.
Lile kundi lilikutana na kupitia njia za mkato ambapo walitokea maeneo ya mtaa wa Jangwani kuelekea barabara ya Msimbazi ndipo polisi walipowabaini na kuwatupia mabomu ya machozi na kusababisha mwanafunzi mmoja kuzimia.

Kariakoo

Maduka mengi katika eneo la Kariakoo yalifungwa kwa hofu ya kuvamiwa na kuibiwa bidhaa na waandamanaji hao.
Mwananchi lilifika katika maeneo hayo muda wa saa 7.00 mchana na kukuta eneo hilo likiwa na watu wengi kama ilivyo kawaida.
Watu mbalimbali ambao hujipatia kipato kutokana na shughuli mbalimbali sokoni hapo walilaani kufungwa kwa biashara siku ya jana wakisema kuwa inawafanya wakose kipato cha siku.
“Hawa waislamu wanatukosesha uhuru wa kufanya kazi, mpaka sasa walau mtu ungekuwa umapata chochote kwa kazi zetu lakini maduka yamefungwa na sisi tunakosa kazi” alisema mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Muddy ambaye ni mbeba mizigo wa soko la Kariakoo.

Shule zafungwa

BAADHI ya shule zilizopo katikati ya jiji zililazimika kusitisha masomo jana kwa kuhofia maandamano hayo. Miongoni mwa Shule zilizofungwa ni pamoja na Shule ya Msingi Bunge
 

Hata hivyo, eneo hilo lilikuwa na ulinzi wa kutosha kwani baadhi ya barabara za kuelekea katika ofisi hiyo zilikuwa zimefungwa na hakuna mtu  yeyote  aliyekuwa akikatiza katika eneo hilo.Magari pia hayakuwa yakipita katika eneo hilo.
Katika kuimarisha ulinzi, Polisi  walilazimika kutumia pikipiki, magari na mbwa kufanya doria katika maeneo yaliyo karibu na ofisi ya DPP.
 

Kadhalika, Polisi walikuwa wanatumia magari binafsi ambayo ndani yake kulikuwa na askari  waliovalia kiraia jambo ambalo lilisaidia kuwakamata baadhi ya waandamanaji kiurahisi. Kutokana na hilo kila kiku
ndi kilichojaribu kupita kuelekea kwa DPP kilikamatwa.
Hadi saa 11 jioni waandishi wa habari walipoondoka katika eneo hilo bado kulikuwa na ulinzi mkali.
 

Mnazi mmoja
Maandamano hayo yaliyokuwa na sura mpya ya kimya kimya tofauti na ilivyozoeleka,yalifanikiwa kupenyeza mpaka eneo la Mnazi Mmoja huku askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) wakiendelea kuwadadisi wahusika wote waliokuwamo katika maandamano hayo.
Magari ya kikosi hicho yalikuwa yakizunguka katika maeneo hayo kwa lengo la kusitisha  maandamano.
 

Maandamano hayo yaliyokuwa na idadi kubwa ya vijana huku wakiwa wamevaa mavazi ya kawaida  hatua iliyowachanganya askari hao kufanya maamuzi ya kuwatawanya.
Zaidi ya saa tatu,  hofu ilikuwa vimetanda miongoni mwa wakazi waliokuwa katika shughuli zao mbalimbali za kijasiriamali kuanzia maeneo yote ya Mnazi mmja,Kariakoo na Posta.
 

Katika Mitaa hiyo juhudi za askari wanaotumia usafiri wa pikipiki walifika eneo hilo na kuwakamata zaidi ya waandamanaji 15 walikuwa mstari wa mbele huku wengine wakitawanyika kwa njia za vichochoroni ili kutimiza lengo la kufika kwa DPP.
Katika maeneo mengine ni pamoja na mitaa ya kituo cha Akiba baada ya askari kuvamia na kuwakamata waandamanaji hao.
 

Askari hao waliokuwa wametanda kila kona katika maeneo hayo ili kuhakikisha wanafanikiwa kuzuia maandamano ya wafuasi.
Mmoja kati ya waliokamatwa katika purukushani hilo,ni mwandishi wa habari kutoka chombo  kinachadaiwa kurusha matangazo ya kiislamu (jina halikufahamika mapema) baada ya kujichanganya katika kundi la waandamanaji hao bila kuwa na kitambulisho chochote
Habari hii imeandikwa na Aidan Mhando, Aisha Ngoma, Pamela Chilongola, Julius Mathias ,Bakari Kiango, Kelvin Matandiko

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate