KAMPUNI ya Ndege ya Precision Air,imemteua Sauda Rajab kuwa
Ofisa Mkuu Mtendaji(CEO) wa kampuni hiyo na uteuzi wake unaanza Machi
Mosi mwaka huu.
Sauda anatokea Shirika la Ndege la Kenya Airways ambako alikuwa Meneja Mkuu wa Kitengo cha Mizigo.
Amefanya kazi katika shirika hilo kwa miaka 23.
Anachukua nafasi ya Alphonce Kioko, ambaye ameshikilia wadhifa huo kwa miaka 10.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na Mwenyekiti wa Bodi ya Precision Air, Michael Shirima, ilisema Sauda ameweka rekodi ya kuwa mwanamke wa kwanza kuongoza shirika la ndege Tanzania.
Sauda anatokea Shirika la Ndege la Kenya Airways ambako alikuwa Meneja Mkuu wa Kitengo cha Mizigo.
Amefanya kazi katika shirika hilo kwa miaka 23.Anachukua nafasi ya Alphonce Kioko, ambaye ameshikilia wadhifa huo kwa miaka 10.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na Mwenyekiti wa Bodi ya Precision Air, Michael Shirima, ilisema Sauda ameweka rekodi ya kuwa mwanamke wa kwanza kuongoza shirika la ndege Tanzania.
“Tuna imani Sauda ataleta mtazamo mpya wa kiutawala kwa Precision Air na kusaidia kukua zaidi na kujenga ushindani kwa kampuni kubwa za usafiri wa anga duniani.
“Anao uwezo wa kujenga katika msingi ambao tayari Kioko na wafanyakazi wengine wameweza kuujenga.,” alisema Shirima.
Shirima alieleza kuwa Sauda ameahidi kutimiza majukumu yake vyema baada ya kutembelea katika vitengo mbalimbali na kupania kuongeza tija kwenye kampuni hiyo.
Kioko amestaafu akiwa ameitumikia kampuni hiyo kwa miaka 10 tangu alipojiunga na Precision Air na kuijenga kampuni na kuipa mafanikio makubwa.
Sauda anachukua la kuiongoza Precision Air katika kipindi hiki ambacho kuna ushindani mkali katika sekta ya usafiri wa anga nchini Tanzania kutokana na kuibuka kwa mashirika kadhaa ya ndege.
No comments:
Post a Comment