Uchunguzi uliofanyika hivi karibuni nchini Marekani unaonesha kuwa,
tangu mwaka 2009 kwa uchache mauaji mamoja ya watu wengi kwa mpigo
yanatokea kila mwezi nchini humo.
Uchunguzi huo ulioendeshwa na watafiti
wa Mayors Against Illegal Violence kwa kuangalia data za polisi ya FBI
na ripoti za vyombo vya habari katika kila tukio la mashambulizi
yaliyopelekea watu wengi kuuawa kwa mpigo tangu mwezi Januari mwaka 2009
unaonesha kuwa, pamoja na mambo mengine, kuna kesi 43 za mauaji
yaliyosababishwa na ufyatuaji risasi na kuua watu wengi kwa mpigo
zilizofanywa na watu waliobeba silaha waliovamia maeneo ya uma katika
majimbo 25 ya Marekani katika kipindi hicho cha miaka minne iliyopita
jambo ambalo linaonesha kuwa kwa kila mwezi kwa uchache kesi moja ya
mauaji kama hayo inatokea nchini Marekani.
Hayo yaliripotiwa jana na
gazeti la Washington Post na kuongeza kuwa, mashambulizi ya namna hiyo
ni sehemu ndogo tu ya vifo vinavyotokea Marekani kwa kutumia mabavu. Kwa
mujibu wa uchunguzi huo, kesi hizo zinajumuisha yale mashambulizi
ambayo kwa uchache yamepelekea watu wasiopungua wanne kuuawa kwa mpigo.
Chanzo Idara ya Iran kiswahili Radio
No comments:
Post a Comment