TAASISI isiyo ya kiserikali ina yojishughulisha na masuala ya
Madeni ya Taifa na Maendeleo (TCDD), imesema Serikali ya Tanzania ndiyo
inaongoza kwa kukopa zaidi, ikieleza kuwa kati ya mwaka 2008 hadi mwaka
2011, imekopa kiasi cha Sh15trilioni na kufanya deni la taifa kufikia
Sh21trilioni.
Add caption |
Rais Kikwete aliingia madarakani mwaka 2005, baada ya rais aliye mtangulia, Benjamin Mkapa kumaliza kipindi chake cha uongozi wa miaka 10 kilichoanzia mwaka 1995 hadi mwaka 2005.
TCDD imebainisha kuwa Serikali inakopa fedha hizo kutoka Benki Kuu (BoT), Benki za Biashara, Kampuni za Bima na Mashirika ya Hifadhi za Jamii. Pia inakopa katika taasisi za kimataifa ikiwamo, Benki ya Dunia (WB), Benki ya Maendeleo Afrika (ADB) na Shirika la Fedha Duniani (IMF).
Katika maelezo yake, Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi hiyo Hebron Mwakagenda, alisema kuwa kite ndo cha Serikali kukopa fedha kwa ajili ya matumizi yasiyo muhimu pamoja na kuwalipa watumishi wake mishahara, ndiyo sababu ya kukua kwa deni hilo la taifa.
“Serikali ya awamu ya nne imekopa kwa kiwango kikubwa, kwani tangu iingie madarakani imeshakopa Sh15trilioni, sasa sijui mpaka inamaliza muda wake itakuwa imekopa kiasi gani?” alisema Mwakagenda akihoji na kuongeza;
“Hata kama kukopa ni kuzuri basi tukope na fedha tuzifanyie mambo ya maana hasa katika maendeleo, tukope tu pale inapokuwa lazima kufanya hivyo.”
TCDD imeeleza kwamba hali hiyo ni hatari, hasa
ikizingatiwa kuwa miaka kadhaa iliyopita, Tanzania kupitia Mpango wa
Nchi Maskini zenye Madeni Makubwa (HIPC), ilifutiwa kiasi kikubwa cha
madeni, lakini sasa imeanza kukopa tena na deni kukua kwa kasi.
Taasisi hiyo pia imesema kitendo hicho kimechangia kuporomoka kwa uchumi wa taifa kunakosababishwa na riba kubwa za mikopo hiyo, ambapo kulingana na idadi ya Watanzania ukigawanya deni hilo kwa wote, inaonyesha kuwa kila Mtanzania anadaiwa wastani wa Sh450,000.
Mwakagenda, ambaye taasisi yake inafanya kazi ya
kuishauri Serikali katika suala zima la deni la taifa na maendeleo,
alisema hadi kufikia Oktoba mwaka jana, deni la nje lilikuwa Sh15.9
trilioni.
Kwa mujibu wa taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu
wa Hesabu za Serikali (CAG), aliyoitoa bungeni mjini Dodoma mwaka jana,
taifa linapoteza Sh3 trilioni katika ukwepaji wa kodi na ubadhirifu,
huku akishauri kuwa mambo mawili yakifanyiwa kazi deni hilo litapungua
au kumalizika kabisa.
“Deni linakuwa kwa kiasi kikubwa na tunakopa katika mabenki ya biashara, ambayo riba yake ni kubwa, fedha nyingi zinazokopwa hutumika kulipa mishahara,” alisema Mwakagenda.
Alifafanua kwamba mwaka 2007 hadi 2008 deni la
taifa lilikuwa Sh6.4 trilioni na kwamba, kuanzia mwaka 2007 hadi 2011
deni hilo limeongezeka hadi Sh21 trilioni.
Nini kifanyike
Alisema jambo walilofanya kama TCDD ni kutoa mapendekezo kwamba Katiba ijayo iwe na kipengele kitakachoeleza kiwango cha ukomo wa kukopa (debt ceiling).
Alisema deni ni utumwa na fedheha na kwamba nchi inatakiwa
kukopa kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu, kwamba ifanye hivyo kama
itashindwa kabisa kupata namna nyingine ya kugharimia maendeleo.
“Ukopaji katika benki za biashara zinazotoa riba
kubwa kwa ajili ya kulipia matumizi ya kawaida ni hatari kwa taifa na
kwa vizazi vya sasa na baadaye,” alifafanua.
Nini kifanyike
“Kama taifa, tukijipanga zaidi katika kuboresha
usimamizi katika sekta mbalimbali sambamba na kusimamia mapato na
ulipaji kodi, hatutakopa tena katika mabenki ya biashara,” alisema na
kuongeza:
“Hata ukitazama ongezeko la deni hili la taifa, ni
sawa na Sh3 trilioni kila mwaka, fedha ambazo kwa mujibu wa taarifa ya
CAG zinapotea kila mwaka.”
Alifafanua kwamba hilo li nawezekana iwapo
Serikali itaongeza wigo wa kudhibiti misamaha ya kodi, kuziba mianya ya
ukwepaji kodi na kuangalia kwa makini sekta mpya kama za madini, gesi na
utalii kuliko kukazana kukopa kama njia pekee ya kuendesha shughuli za
maendeleo.
“Tunataka Serikali ifungue macho na kuona fursa
mpya za kupata mapato ya ndani badala ya kugeuza mikopo kuwa ndiyo
suluhisho la kudumu la mipa ngo yetu ya maendeleo,” alisema Mwakagenda.
Alisema jambo walilofanya kama TCDD ni kutoa mapendekezo kwamba Katiba ijayo iwe na kipengele kitakachoeleza kiwango cha ukomo wa kukopa (debt ceiling).
Januari 4 mwaka huu Mwakagenda aliliambia gazeti
hili kwamba deni hilo ni kiwango cha juu kabisa kwa nchi kuweza kukopa
kutoka kwenye masoko ya kimataifa. Deni limeongezeka kwa dola 456.1
milioni katika ki pindi cha mwaka mmoja tu tangu Oktoba 2011.
Alisema taarifa za Benki Kuu ya Tanzania
zinaonyesha kuwa deni la ndani limefikia Sh5.1 trilioni hadi kufikia
Oktoba mwaka jana na kwamba kiasi hicho ni sawa na ongezeko la Sh513
bilioni tangu mwaka 2011.
Alisema zipo fedha zinazotumika kujenga barabara,
madaraja, majengo mbalimbali ya shule na vyuo, lakini kinachotakiwa ni
Serikali kufikiri mara mbili kabla ya kuamua kukopa na kuzitumia fedha
hizo za mkopo.
Katika mapendekezo yao, Mwakagenda alisema
wameitaka Serikali kuwa na nidhamu katika kukopa kwa kuwa deni hilo
limevuka kiwango cha kimataifa.
Maelezo ya Wizara
Maelezo ya Wizara
Katika ufafanuzi wake, Mwakagenda alisema baada ya
kuwasilisha kwa Serikali kiwango hicho cha deni la taifa, Gavana wa
Benki Kuu (BOT), Profesa Beno Ndulu alitoa takwimu kwamba hali ya deni
siyo mbaya na kwamba imefikia asilimia 19, kiwango ambacho kinakubalika
kimataifa kukopa tena.
“Waziri wa Fedha na Uchumi, Dk William Mgimwa yeye
alitueleza kuwa bado tunakopesheka, lakini pamoja na hayo hatukubaliani
na kauli ya Serikali kwa kuwa katika kipindi cha miaka mitano, deni
limekuwa kwa kiwango kikubwa” alisema Mwakagenda.
CHANZO MWANANCHI
No comments:
Post a Comment