Takriban asilimia tisini ya wanwake katika kijji kimoja inasemekana wameondolewa mfuko wao wa uzazi
Wakereketwa wa haki za
kibinadamu wanasema kuwa maelfu ya wanawake wamekuwa wakiondolewa mfuko
wa uzazi kwa ulaghai ambapo wanadanganywa kuwa watashikwa na saratani
iwapo hawafanyiwi hivyo katika kliniki za kibinafsi.

Kuongezeka kwa visa vya wanawake kuondolewa mfuko wa uzazi, ni kutokana na ongezeko la kliniki na hospitali za kibinafsi katika miaka ya hivi karibuni.
Zote hizo zinajaza pengo la mfumo duni wa serikali hususan katika maeneo ya vijijini.
Wanaharakati wanataka hospitali hizo kuchunguzwa na hata kuwekewa sheria za utenda kazi ili kuhakikisha kuwa haziwanyanyasi akina mama maskini.
Daktari Narendra Gupta anayefanya kazi katika shirika moja lisilo la kiserikali, Prayas anasema kuwa madaktari wa kibinafsi, wameona fursa ya kutengeza pesa kwa haraka.
Anaelezea kuwa kuna mbinu nyingi tu ambazo, mfuko wa uzazi unaweza kuondolewa bila upasuaji, na kwamba hiyo inapaswa kuwa tu njia ya mwisho katika matibabu yoyote.

Mmjoa wa wanawake walioondolewa mfuko wao wa uzazi
Lakini jambo la kushangaza ni kuwa wasichana wadogo wanaondolewa mfuko huo baada ya madakrati kuwatisha kuwa watapata saratani ikiwa hautaondolewa.
Waziri wa ustawi wa vijijini Jairam Ramesh, anasema kuwa changamoto kubwa ni kuwa mfumo wa serikali umeporomoka na kwamba watu hulazimika kwenda katika hospitali za kibinfasi,
Anasema kuwa kwa hilo watu hulazimika kutumia pesa nyingi sana na hata kupata matibabu wasiyoyahitaji.
No comments:
Post a Comment