
BURKINA FASO imeing’oa Ghana kwa mikwaju ya penalti katika nusu fainali ya kombe la mataifa ya Afrika kufuatia sare ya 1-1 hadi kumalizika dakika 120 za mchezo.
Goli
la Ghana lilifungwa na Mubarak Wakaso kwa njia ya penalti katika dakika
ya 13, baada ya mshambuliaji wa Ghana Atsu kuangushwa katika eneo la
hatari.
Burkina Faso wakasawazisha kupitia kwa Aristides Bance katika dakika ya 60 ya mchezo.
Mpambano ulimaliza dakika 90 kwa sare ya bao 1-1. Hivyo kulazimika kuongezwa dakika 30.
Katika
kipindi hicho cha nyongeza Burkina Faso ndiyo ilifanya mashmbulizi
mengi zaidi katika lango la Ghana, ambapo goli lililokuwa limefungwa na
Burkina Faso kipindi hicho cha nyongeza, lilikataliwa kwa madai ya
mfungaji kumchezea vibaya mlinzi wa Ghana.
Katika hatua ya mikwaju ya Penalti, Burkina Faso ikafanikiwa kupata 3-2.
Kwa
matokeo hayo, Burkina Faso inayoshika nafasi ya 92 kwa ubora duniani,
sasa itaumana na Nigeria katika fainali zitakazochezwa Jumapili katika
Uwanja wa Taifa wa Johannesburg.
Nigeria ilifanikiwa kuichapa Mali 4-1 katika nusu fainali nyingine iliyochezwa mapema Durban.
Ghana itacheza na Mali Jumamosi huko Port Elizabeth katika mechi ya kuwania nafasi ya tatu.Via saluti 5
No comments:
Post a Comment