EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Wednesday, March 27, 2013

Dk Slaa awatuhumu Usalama wa Taifa

 
Dar es Salaam. 
Kwa ufupi
“Chadema ni chama makini na hakiwezi kuyumbishwa na mtu yoyote wala idara yoyote inayotumiwa na baadhi ya watu ili kutaka kukizohofisha,” alisema Dk Slaa ambaye mara kwa mara amekuwa akilalamika kuchezewa rafu.
Dar es Salaam. Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk Willibrod Slaa ameanza kuisakama Idara ya Usalama wa Taifa kuwa wanatumia mbinu mbalimbali kuwahujumu na kwamba mbinu zinazofanywa na idara hiyo ni kueneza propaganda walizodai za uongo dhidi yao.

Akizungumza jana makao makuu cha chama hicho jijini Dar es Salaam, Dk Slaa alisema: “Tumezibaini mbinu zinazofanywa na Usalama wa Taifa kwa kutumiwa na CCM kueneza propaganda za uongo dhidi yao kwa lengo la kukichafua chama, lakini haziwezi kufanikiwa kwani tayari tumegundua mbinu zao.”

“Chadema ni chama makini na hakiwezi kuyumbishwa na mtu yoyote wala idara yoyote inayotumiwa na baadhi ya watu ili kutaka kukizohofisha,” alisema Dk Slaa ambaye mara kwa mara amekuwa akilalamika kuchezewa rafu.

Hata hivyo, viongozi wanaohusika na idara hiyo akiwamo Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utawala Bora), George Mkuchika walipotafutwa na gazeti hili kwa nyakati tofauti ili kuzungumzia tuhuma hizo za Dk Slaa, hawakuwa tayari kuzizungumzia.

Waziri Mkuchika alisema asingeweza kuzungumzia tuhuma hizi kwa kuwa hakuwa amezisikia wala hafahamu ni ujumbe upi uliomo katika kauli ya Dk Slaa.

“Mimi nimeshinda kwenye Kamati ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala tangu asubuhi na sasa ndiyo natoka, kwa hiyo sijasikia hiyo kauli wala huo mkutano wa (Dk Slaa). Kwa hiyo siwezi kujibu chochote kwa sasa,” alisema Mkuchika na kuongeza:

“Nadhani tumeelewana na pengine tusubiri pindi nitakapofahamu ni kipi amekizungumza na nikafanyia uchunguzi tutaona kama kuna cha kujibu basi tutajibu wakati huo, lakini kwa sasa siwezi kusema chochote.”

Mapema gazeti hili lilimtafuta Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa, Rashid Othman ili kuzungumzia madai hayo ya Chadema lakini mara zote simu yake ilikuwa haipatikani.

Baadaye Mwananchi iliwasiliana na Naibu Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa, Jacky Nzoka ambaye alijibu kwa kifupi na kukata simu: “Mimi siyo msemaji tafadhali.”

Hata hivyo, katika tuhuma hizo Dk Slaa alisema mifano hai ipo kwake kwani kila wakati amekuwa akizungukwa na watu wa idara hiyo kwa malengo yao binafsi, lakini malengo yao hayawezi kufanikiwa kwani wao wapo makini katika hilo.

“Mimi kila wakati Usalama wa Taifa wamekuwa wakinizunguka zunguka kwa mambo yao binafsi wanayoyafuatilia kwangu, lakini nataka niwaambie kwamba nimewagundua na mbinu zao haziwezi kufanikiwa ila nawataka wasichoke kunifutalia na waendelee tu,” alisema.

Chadema na Sh400 milioni
Dk Slaa alikiwakilisha Chadema kusaini mkataba wa ushirikiano na Chama cha Konservative cha Denmark ili kuinua uwezo wa vijana na wanawake kisiasa.

Chama hicho kimeahidiwa kupewa Sh400 milioni kwa ajili ya kutoa mafunzo ya kujiimarisha kisiasa kwa Baraza la Vijana la chama hicho (Bavicha) na lile la Wanawake (Bawacha).

Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk Willibrod Slaa ameanza kuisakama Idara ya Usalama wa Taifa kuwa wanatumia mbinu mbalimbali kuwahujumu na kwamba mbinu zinazofanywa na idara hiyo ni kueneza propaganda walizodai za uongo...Alisema mafunzo hayo yatatolewa kwa watu 900 wa Bavicha na 900 wengine kutoka Bawacha na yanatarajia kuanza siku chache zijazo hadi Desemba mwaka huu yakiwa na lengo la kuwajengea uwezo wa kisiasa vijana wa Chadema na wanawake ili kuhakikisha wanaimarika kisiasa Tanzania,” alisema Dk Slaa.

Akizunguza wakati wa kusaini mkataba huo, Mwenyekiti wa Kamati ya Kimataifa ya Chama cha Conservative, Rolf Aagaard-Svendsen alisema lengo la ushirikino wao ni kuwajengea uwezo wa kisiasa vijana ili washiriki vizuri katika medani za kisiasa

Gazeti la Mwananchi ndo chanzo cha habari hii.

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate