MTU
mmoja ambaye anasadikiwa kuwa ni jambazi ameuawa kwa kupigwa risasi na
Askari wa Jeshi la Polisi akiwa kwenye harakati za kuteka magari katika
Eneo la Mlima Nyoka Jijini Mbeya baada ya kutokea kwa majibizano ya
kurushiana risasi.
Jambazi
huyo ni miongoni mwa watu waliokuwa wakitafutwa na Jeshi la Polisi
Mkoani hapa akituhumiwa kuhusika na mauaji ya Askari Polisi mwenye namba
G 68 PC Jafari yaliyotokea Februari 6, Mwaka huu katika eneo la
Matundasi Wilayani Chunya.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Mbeya Diwani Athumani amethibitisha kutokea kwa tukio
hilo katika Mkutano alioufanya na waandishi wa Habari Ofisini kwake
ambapo alisema tukio hilo lilitokea jana majira ya Saa 10(kumi)
Alfajiri
Kamanda
Diwani alisema kabla ya tukio majambazi wapatao wanne tayari walikuwa
wameweka mawe barabarani kwa nia ya kuteka magari ili wafanye uporaji
katika eneo hilo la Mlima Nyoka ambalo limekuwa na matukio kadhaa ya
watu kuporwa mali zao.
Alisema
Jeshi la polisi baada ya kupata habari za kutegwa mawe, askari walifika
kwa wakati kwa kuwa polisi walikuwa jirani na eneo hilo na kuweka mtego
kwa kuwa majambazi hawakuwa wameonekana kwa wakati ule.
Aliongeza
kuwa baada ya muda majambazi walipoona taa za gari walijitokeza tayari
kushambulia lakini kabla ya hapo polisi walitoa amri ya kujisalimisha
kinyume chake wakaanza kupiga risasi ovyo ndipo mashambulizi ya polisi
yakafanywa.
Diwani
alisema katika mapambano hayo alijeruhiwa jambazi mmoja kwa risasi
kiunoni na ubavuni kulia na wengine watatu walifanikiwa kutoroka ambapo
Marehemu alipowahishwa hospitali kwa matibabu daktari alibaini kuwa
amekwisha fariki.
Mwili wa Jambazi sugu Emanuel Blasius Mdendemi ukiwa umehifadhiwa katika hospitali ya rufaa Mbeya
Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya Diwani akiangalia mwili jambazi lililouwawa na kikosi cha polisi Mbeya
Baadhi ya polisi na waandishi wa habari wakiwa nje yajengo la kuhifadhia maiti katika hospitali ya rufaa Mbeya
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Diwani Athumani amethibitisha kutokea kwa tukio hilo katika Mkutano alioufanya na waandishi wa Habari Ofisini kwake ambapo alisema tukio hilo lilitokea jana majira ya Saa 10(kumi) Alfajiri
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Diwani Athumani akionyesha baadhi ya siraha alizokutwanazo jamabazi huyo aliyeuwawa
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Diwani Athumani akionyesaha hirizi iliyofungwa katika bunduki aliyokuwa anatumia jambazi huyo kama kinga katika matukio yake
Hii ndiyo hirizi iliyofungwa katika bunduki aliyokuwa anatumia jamabazi huyo jamani waganga wakienyeji acheni hizo kuwadanganya watu matokeo yake ni kuongeza uhalifu nchini hakika nao tutawashughulikia kwani wamekuwa chanzo cha uhalifu nchini hayo yamesemwa na kamanda Diwani
Kamanda Diwani akiongea na waandishi wa habari
Alisema
jambazi huyo alikutwa na silaha moja SMG yenye namba AB huku namba
nyingine zikiwa zimefutwa na magazine yake ikiwa na risasi ishirini na
mbili (22) pamoja na mapanga mawili([2).
Aliongeza
kuwa baada ya Marehemu kufanyiwa upekuzi maungoni mwake jambazi huyo
alikutwa na kitambulisho cha mkazi chenye namba B.0010453 chenye jina la
Emanuel Blasius Mdendemi aliyezaliwa mwaka 1984 eneo la Matamba
wilayani Makete Mkoa wa Iringa makazi yake ni Uwemba Mkoani Njombe.
“Jambazi
huyu amebainika kuwa ni miongoni mwa majambazi waliokuwa kwenye mtandao
wa majambazi uliokamatwa hivi karibuni kuhusiana na matukio waliyofanya
Mikoa mbalimbali ikiwemo Mbeya,Njombe na Iringa.aidha amebainika
kushiriki katika tukio la mauaji ya askari polisi PC Jafari wa kituo cha
Mkwajuni – Chunya tarehe 06.02.2013.” Alisema Kamanda Diwani.
Aliongeza
kuwa ufuatiliaji wa majambazi waliotoroka unaendelea kufanywa ambapo
pia anatoa wito kwa yeyote mwenye taarifa za wahalifu hao azitoe bila
kuchelewa kwa jeshi la polisi ili zifanyiwe kazi.
Pia
amewatahadhalisha majambazi na wahalifu wa makosa yeyote kuachana na
uhalifu kwa kuwa ni biashara isiyo na faida badala yake wafanye shughuli
halali kupata maendeleo ambazo fursa zake ni nyingi.
Picha na Mbeya yetu
No comments:
Post a Comment