KWA
kuwa migogoro ni moja kati ya mambo yanayotokea katika safari ya maisha
si vibaya tukajifunza namna ya kuikabili. Kwa bahati mbaya tafiti
zinaonyesha kuwa kiwango cha migogoro ni kikubwa miongoni mwa jamii
ukilinganisha na watu wenye ufahamu wa kuitatua.
Watu
wamekuwa wakifanyiana ukatili, nchi zikipigana vita kwa sababu ya
migogoro mbalimbali ambayo ingepata wajuzi wa kuitatua isingeleta
madhara makubwa. (L. Ron Hubbard Mtafiti wa Sayansi ya Jamii kutoka
Marekani anathibitisha hili pia).
Zifuatazo ni mbinu za kufikia makubaliano na mtu uliyekosana naye.
Zifuatazo ni mbinu za kufikia makubaliano na mtu uliyekosana naye.
KWANZA : Mgogoro unapotokea baina ya mtu na mtu au taifa kwa taifa kitu
cha kwanza kabisa kufanyika ni kwa wahusika kutambua kuwa wameingia
katika mgogoro na hivyo kutazama kwa kina madhara ya mgogoro na kuamua
kutuliza jazba zao kwa lengo la kutazama namna ya kumaliza matatizo kwa
njia ya amani.
Katika hatua hii hawatakiwi kutafuta nani mwenye makosa katika mgogoro huo bali ni wakati wa kuamua kukaa katika meza ya mazungumzo huku suala la nani mwenye makosa likishughulikiwa baadaye.
Katika hatua hii hawatakiwi kutafuta nani mwenye makosa katika mgogoro huo bali ni wakati wa kuamua kukaa katika meza ya mazungumzo huku suala la nani mwenye makosa likishughulikiwa baadaye.
PILI : Mahali penye mgogoro kila mtu hupenda kusikilizwa, akiamini kuwa
ana sababu za msingi zilizomfanya akasirike au akorofishane na
mwenzake. Hivyo kwa mtu mwenye elimu na nia ya kutatua mgogoro atakuwa
tayari kutoa nafasi kwa upande wa pili utoe dukuduku hata kama litakuwa
limesheheni matusi na uongo. Usimkatize mwenzako anapotoa maelezo yake,
nyamaza umsikilize mpaka mwisho akimaliza na wewe eleza yako.
TATU :
Usikimbilie kujihukumu hasa pale wasuluhishi wanapojaribu kuchambua
mambo kwa kuonesha dalili za kukuzonga na pengine kukuhukumu. “Oke, kama
mimi nina makosa basi niacheni kaeni ninyi wasafi” Usiseme hivyo,
vumilia lawama na pointi yako ya msingi iwe ni kwenye busara ya kulimaza
tatizo.
NNE : Unapokuwa katika safari ya kutaka suluhu, pendelea
sana kuunga mkono yale yanayozungumzwa kwenye kikao au anayozungumza
mwenzako. “Ni kweli kabisa, hapo umesema sawa, nakubaliana na wewe”
Kauli za kukubali kama hizi zina nguvu kubwa ya kuwafanya wajumbe au
mgomvi mwenzako anyonywe hasira na kukuona ni mtu mwelewa unayestahili
suluhu.
TANO: Kama utaona mgomvi wako bado amejaa hasira kiasi cha
kutotaka kukusikiliza, sitisha mapatano na umruhusu aondoke au wewe
uachane naye kwa muda. “Naona bado una hasira nyingi, tulia hasira
zikipungua tutazungumza.”
Unapompa mwenzako muda zaidi wa kutafakari kiwango cha hasira hushuka na pengine kufikiria kwa kina madhara ya kugombana. Usilazimishe suluhu wakati wa muwako wa hasira, ukifanya hivyo utakuza tatizo.
Unapompa mwenzako muda zaidi wa kutafakari kiwango cha hasira hushuka na pengine kufikiria kwa kina madhara ya kugombana. Usilazimishe suluhu wakati wa muwako wa hasira, ukifanya hivyo utakuza tatizo.
SITA: Mtakapofikia katika hatua za maelewano
na ukabaini kuwa wewe ulikuwa na makosa katika mgogoro huo, uungwana
unakutaka uwe mwepesi kukiri kosa na kutaka kumaliza tatizo. “Niliteleza
naomba unisamehe.” Lakini hata kama umeona mwenzako ana makosa ila
hataki kukubaliana na wewe, kuwa tayari kubeba lawama kwa lengo la
kumaliza tatizo.
SABA: Jambo kubwa la mwisho linaloweza kusaidia
kutatua migogoro ni kutumia nguvu ya ufahamu wako wa mambo. Kwa mfano;
kama unaishi na mkeo ama ndugu kwenye nyumba moja unatakiwa kumfahamu
tabia zake na kuzichukulia hadhari, vivyo hivyo bosi wako, wafanyakazi
wenzako, wanafunzi wenzio, waalimu wako, lazima uwafahamu tabia zao. Hii
itakusaidia kutoingia katika mgogoro nao.
No comments:
Post a Comment