EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Friday, March 22, 2013

JK aziponda Simba, Yanga

RAIS Jakaya Kikwete amezipiga ‘kijembe’ klabu kongwe hapa nchini, Simba na Yanga, kutokuwa na maendeleo kisoka na kuiacha Azam FC, ikiwapiga kumbo kila idara huku wao wakiendekeza ushirikina mbele na migogoro.
Kikwete aliyasema hayo jana, wakati akiweka jiwe la msingi la klabu ya Azam iliyoko Chamazi nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.

Rais aliipongeza Azam kwa hatua ambayo imefikia, licha ya kuwa na uchanga katika soka na kuzipita klabu za Simba na Yanga.

Alisema endapo Azam inataka kupiga hatua na kuifikisha nchi mbali kwa kulitangaza jina la Tanzania, ifanye mambo yake bila kuzifuata timu kongwe na kudai kuwa itafika mbali kitaifa na kimataifa pia.
“Naamini mna uwezo wa kufika mbali katika ulimwengu wa soka, ila msiwe karibu na hizi timu, mtajikuta mnaishia hapahapa; wao mechi mechi moja wanatolewa,” alisema Kikwete na kuwafanya watu walioshuhudia hafla hiyo kuvunjika mbavu.
Aidha Kikwete alisema kutokana na mafanikio ambayo Azam wameyapata hadi sasa, ikiwemo uwanja na mambo mengine, imeonekana kama wao ndio vigogo na kusababisha kuogopwa na jamaa ambao wanajifanya wakubwa.
 “Mpaka sasa haionekani nani mkubwa, maana kuwa na wanachama wengi sio ishu na nyie nina imani mnaweza kulileta hili Kombe la Shirikisho nyumbani, najua timu kubwa zikiwa na mechi na nyie zinakuwa na wasiwasi, hivyo basi mpaka sasa nyie ndio mtasaidia soka la Tanzania kukua,” alisema Kikwete.

Alikwenda mbali zaidi na kuwataka Azam, kuacha kufuata vivuli vya hizo timu na kujisimamia wenyewe, kwa kuwa timu mbili kongwe zina wanachama wanaopiga kura kwa kuhongwa, sambamba na kutumia muda mwingi kulumbana, wakati hawana kitu wanachoingiza katika timu.

Alisema timu kubwa zikiambiwa kutumia Uwanja wa Chamazi, zinaanza kuleta maneno ya ajabu na kuongeza kuwa ushirikina haufai katika soka, cha muhimu ni kucheza mpira na sio kazi ya kuandaa kamati za ufundi na kushindwa kutazama benchi la ufundi ili kujenga timu.
“Ingekuwa mpira ni ushirikina, basi Afrika tungekuwa mabingwa kila mwaka, kama timu inaona uchawi dili, basi ikusanye wachawi wote dunia nzima ikae nao klabuni kwao tuone!” aliongeza Kikwete.

Aliwataka Azam endapo watakuwa na shida yoyote, wasisite kumjulisha na kudai kuwa ombi lao la kupunguziwa VAT katika bidhaa zao za kisoka, atawasiliana na wahusika ili aweze kulipatia ufumbuzi.
Naye Mkurugenzi wa Azam, Yusuph Bakhressa, alishukuru sana kupata nafasi ya Rais kuzindua mradi wao maalumu, ambao lengo lake ni kukuza na kuendeleza mpira wa miguu nchini.
Alisema hadi sasa wametumia sh bilioni 3 katika mradi huo.
Katika hafla hiyo, Rais aliambatana na mkewe Mama Salma Kikwete, Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara, Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam, Mecky Saidi Sadick, na viongozi mbalimbali.

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate