EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Sunday, March 3, 2013

Kikosi cha Pinda kuchunguza mitihani hiki hapa

WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda, ametangaza kikosi kazi kinachounda tume itakayochunguza chanzo cha  kufeli kwa asilimia 60.5 ya watahahiniwa wa Mtihani wa Kidato cha IV mwaka jana nchini.
 
Tume hiyo inayoundwa na watu mbalimbali wakiwamo wabunge, wasomi, viongozi kutoka taasisi za kidini na wadau wa elimu, ilitangazwa jana jijini Dar es Salaam na itaongozwa na Katibu Mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu nchini, Profesa Sifuni  Mchome.
Waziri Mkuu Pinda aliwataja wajumbe wengine wa tume hiyo kuwa ni pamoja na James Mbatia Mbunge wa kuteuliwa, Bernadetha Mshashu Mbunge wa Viti Maalumu na Abdul Marombwa Mbunge wa Kibiti.

Wengine ni Profesa Mwajabu Possi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Honorath Chitanga Makamu wa Rais Chama cha Walimu Tanzania(CWT), Daina Matemu Katibu, Huduma za Jamii na Umoja wa Wakuu wa Shule za Sekondari Tanzania (TAHOSSA).
Wajumbe wengine ni Rakhesh  Rajan, Katibu Mtendaji wa Shirika lisilokuwa na Kiserikali (NGO) Twaweza.

Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki wa Shule na Vyuo Binafsi nchini (TAMONGSCO), Mahmoud Mringo na Mratibu wa Taasisi ya Kukuza Mitalaa, Kizito Lawa.
Wengine ambao watatoka katika taasisi za dini  ni  Peter Maduke ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji Shirika la Kikristo la Huduma za Kijamii  (CSSC), Nurdin Mohamed Mkuu wa Chuo cha Ualimu Alharamain iliyopo chini ya Baraza la Waislamu Tanzania (Bakwata).


Wajumbe wa kutoka Zanzibar ni  Suleiman Hemed Khamis mjumbe  kutoka Baraza la Wawakilishi, Abdalla Hemed Moh’d wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA ) na  Mabrouk Jabu Makame  wa Baraza la Elimu Zanzibar.
Akitangaza kuundwa kwa tume hiyo Pinda alisema matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Nne mwaka 2012, yameonyesha kuwa kiwango cha ufaulu kimeshuka kwa kiasi kikubwa, ikilinganishwa na mwaka 2011.

Matokeo hayo yameonyesha kuwa kati ya wanafunzi 397,132 waliofanya mtihani huo, watahiniwa 126,851 ndiyo waliofaulu.

“Katika idadi hii ya wanafunzi waliofaulu katika daraja la kwanza hadi la tatu ni 23,520 na daraja la nne ni 103,327. Watahiniwa 240,903 sawa na asilimia 65.5 wamepata daraja 0,” alisema Waziri Mkuu akiongeza:  “Kutokana na matokeo haya mabaya, Serikali imeamua kuunda tume hii itakayochunguza tatizo hili kwa madhumuni ya kupata ufumbuzi wa kudumu.” 

Alisema kuwa tume hiyo itakuwa na kazi nyingi ikiwa ni pamoja na kubainisha sababu za matokeo hayo kuwa mabaya, kutathmini nafasi za halmashauri katika kusimamia elimu ya sekondari na kuainisha sababu nyingine zinazoweza kuchangia hali ya matokeo hayo.

“ Pia itapaswa kutoa mapendekezo ya hatua za kuchukua mara moja kwa wanafunzi 240,903 waliopata daraja la sifuri katika Mtihani wa Kidato cha Nne mwaka 2012,  pamoja na kupendekeza jinsi ya kukabiliana na mwenendo wa kushuka kwa kiwango cha elimu mara moja, kipindi cha muda mfupi, kati na kipindi cha muda mrefu,” alisema Pinda.
Alisema pia tume hiyo itatathmini uwiano wa mitihani inayotungwa na Baraza la Taifa la Mitihani, uhakiki wake na maswali unaofanywa na Taasisi ya  Elimu pamoja na kutathmini mihutasari iliyotumika kuwaandaa wanafunzi kuanzia kidato cha kwanza hadi cha nne mwaka 2012.

“Tume hii itachunguza pia umahiri wa walimu kumudu maudhui wanayofundisha, mazingira ya kufundisha na kufundishia, matumizi ya vitabu na zana za kufundisha na kujifunzia, pamoja na utoshelevu wa walimu kwa masomo.
Kutathmini mchakato mzima wa usahihishaji na kuangalia usahihi wa alama za karatasi na majibu ya matokeo,” alisema Waziri Mkuu.
Mambo mengine ambayo tume hiyo inapaswa kuchunguza ni pamoja na mwamko wa jamii kwenye elimu, upatikanaji wa chakula cha mchana shuleni, kutathmini mikondo miwili mfumo uliopo Zanzibar na kuangalia upungufu wa miundombinu, ikiwamo madarasa, maabara pamoja na michango ya wazazi na walezi na kutathmini mfumo wa udhibiti wa nidhamu ya walimu.

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate