EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Wednesday, March 20, 2013

Maaskofu wawasha moto mahusiano baina ya Wakristo,Waislamu na msimamo wa serikali.

Wamshambulia Kikwete, wamkumbuka Mwinyi
JUKWAA la Wakristo Tanzania (TCF), limetoa tamko kali kuhusiana na kuzorota kwa mahusiano baina ya Wakristo, Waislamu na msimamo wa serikali.

TCF imeeleza kusikitishwa kwake na mgogoro uliotokea hivi karibuni kuhusiana na nani anastahili kuchinja ambapo wameeleza kuwa wanashindwa kuelewa msimamo wa Rais Jakaya Kikwete na viongozi wengine waandamizi kupata kigugumizi kuhusiana na suala hilo.

“Tumeshindwa kabisa kuelewa msimamo wa Rais Kikwete na viongozi wengine wa serikali. Wakati wa Serikali ya Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi ambaye pia ni Muislamu, ilipotokea ugomvi wa mabucha ya nyama ya nguruwe Dar es Salaam, rais huyo kwa kulinda katiba ya nchi ambayo aliapa kuilinda, alisema mwenyewe kwa nguvu zote kuwa kila mtu ana uhuru wa kula anachotaka na mtu wa dini moja asimhukumu mwingine kwa kile anachokula. Baada ya kusema hivyo hali ikawa ya amani, kwanini Rais Kikwete anapata kigugumizi kuhusu nani achinje?” ilisema taarifa hiyo iliyosaniwa na maaskofu hao.

Tamko hilo lilitolewa kwa niaba ya viongozi wa TCF na Askofu Peter Kitula wa Umoja wa Wakristo (CCT), Askofu Tarcisius Ngalalekumtwa wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) na Askofu Batholomeo Sheggah wa Baraza la Maaskofu wa Makanisa ya Kipentekoste (PCT).Walisema kuwa serikali imekuwa na kigugumizi kuhusu nani achinje, hivyo wanaitaka iweke utaratibu wa kugawana machinjio na mabucha kati ya Wakristo na Waislamu.
“Kila Mtanzania awe huru kujinunulia kitoweo mahali anapotaka na Wakristo wote Tanzania waelewe kuwa hawajavunja sheria yoyote ya nchi wakiamua kuchinja kitoweo chao wenyewe,” lilisema tamko hilo.

Pia walieleza kwa kuwa zipo bidhaa zilizoandikwa neno ‘Halal’ na nyingine zisizo na nembo, hivyo ni dhahiri kuwa vyakula hivyo vimegawanyika kwa kufuata misingi ya imani za dini.
Maaskofu hao pia walisema kuwa wanatambua kuchinja ni ibada ya Waislamu lakini wametaka Wakristo wasilazimishwe kula nyama zilizochinjwa kwa misingi ya ibada ya Waislamu na kuitaka serikali itamke wazi kuwa kila raia ana uhuru wa kufuata imani yake katika suala hilo.

Uchomaji wa makanisa
Kuhusiana na suala la uchomaji wa makanisa ulioambatana na mauaji ya viongozi wa dini, maaskofu hao wamelaani na kueleza kuwa serikali na vyombo vya usalama wa taifa wameshindwa kuchukua hatua kwa wakati, hivyo kuonesha udhaifu na kuliaminisha kanisa kuwa serikali ina ajenda ya siri dhidi ya Ukristo.
TCF imeitaka serikali kutenda haki kwa usawa bila ubaguzi kwani kinachoonekana ni kushindwa kuheshimu katiba juu ya haki za raia hali inayosababisha waamini wa dini ya Kikristo kukosa imani na serikali iliyoko madarakani.
“Jukumu la kulinda raia ni haki ya kikatiba na kisheria, serikali inatakiwa iwalinde raia wake, kama imeshindwa kanisa linataka serikali ikiri hivyo ili kanisa liwaambie wananchi waiwajibishe serikali na viongozi wake kwa kushindwa kutimiza wajibu wake,” walisema maaskofu hao.
Aidha, walisema endapo serikali haitachukua hatua za makusudi, kanisa litachukua hatua ya kuwaambia waamini wake kuwa inaibeba dini moja na kutafakari upya uhusiano wake na serikali.

Pia walitaka serikali kuwahakikishia Wakristo walioko Zanzibar usalama na mali zao kwani wana haki kikatiba.
“Kigezo cha unyanyasaji wa Wakristo walioko Zanzibar ni suala la dini na muungano, inaonekana kama vile Watanzania waliozaliwa Bara hawana haki ya kuishi visiwani, wakati waliozaliwa visiwani wafikapo bara wana haki zote, ni vyema serikali ichukue hatua za makusudi za kuzuia vitisho na mauaji kwa viongozi wa kanisa na Wakristo,” ilisema taarifa hiyo.

TCF ilikutana Machi 8, mwaka huu katika mkutano wa dharura ulioshirikisha maaskofu 177 na kutoa maazimio hayo pamoja na kuwataka Wakristo wote kuwa watulivu na kufunga na kuomba kwa siku saba kuanzia Machi 24 hadi 30, mwaka huu.
Tamko hilo limekuja kufuatia tukio la mchungaji wa Kanisa la Pentecoste Assemblies of God Tanzania (PAGT) Buseresere, Wilaya ya Chato, Mathayo Kachila (45) kufariki dunia huku watu wengine 15 wakijeruhiwa kwa mapanga kufuatia vurugu zilizotokana na mgogoro wa kuchinja.
Katika vurugu hizo nyama ndani ya bucha hiyo ilimwagiwa maji, ikiwamo kuharibiwa kwa madirisha na milango yake.
Tukio lingine ni la Padri Evarist Mushi, ambaye alikuwa paroko wa parokia ya Minara Miwili - Mtoni Zanzibar kupigwa risasi na watu wasiojulikana na kuuawa.
Padri huyo aliuawa wakati akijiandaa kuingia kanisani akitokea kwenye gari yake ambapo ghafla ilitokea gari ndogo na waliokuwamo ndani ya gari ile wakamrushia risasi.
Pia katika tukio lingine makanisa kadhaa yalichomwa moto na Padri Ambrose Mkenda, kushambuliwa na risasi huku kukiwako na vitisho pamoja na vipeperushi vilivyoeleza kuwa kushambuliwa kwa padri huyo sio mwisho wa mapambano.

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate