MANCHESTER
UNITED imeyaaga mashindano ya klabu bingwa Ulaya baada ya kupokea
kipigo cha 2-1 kwenye uwanja wake nyumbani dhidi ya Real Madrid.
United ilikuwa ya kwanza kupata bao baada ya beki wa Real Madrid Sergio Ramos kujifunga dakika ya 48.
Mpira
ulianzia kwa Van Persie upande wa kulia akuupiga mpira na kuokolewa
kabla ya Luis Nani kuunasa na kumpelekea Danny Welbeck ambaye aliupiga
na mpira ukamgonga Ramos na kwenda wavuni huku kipa Dieogo Lopez akiwa
kapotezwa.

Luis Nani akiwafungisha tela mabeki wa Real Madrid
Kabla ya hapo Manchester United walinyimwa goli ambalo lilivuka mstari kabla haujaokolewa.
Dakika ya 57 mwamuzi Cuneyt
Cakir akatoa maamuzi ya kushangaza baada ya kumpa kadi nyekundu ya
utata Luis Nani kwa madai ya kumchezea rafu beki Arbeloa.
Luis
Nani aliruka hewani kuufuata mpira wa juu kwa mguu, wakati anakwenda
juu Arbeloa akawasili na kukutana na mguu wa Luis Nani wakati anashuka
chini na wote wawili wakadondoka na kuugulia maumivu.
Lakini
kwa mshangao wa wengi, Luis Nani alipoinuka akakutana na kadi nyekundu
ya moja kwa moja kutoka kwa mwamuzi huyo raia wa Uturuki mwenye umri wa
miaka 36 na kuanzia hapo mchezo ukabadilika.

Mourinho akimfariji Luis Nani baada ya kutolewa
Real
Madrid waliokuwa wamefichwa kwa kiasi kikubwa wakaanza kusukuma
mashambuli mbele na dakika ya 66 Modrick aliyetokea benchi
akaisawazishia timu yake kwa shuti kali lililogonga nguzo na kujaa
wavuni.
Dakika tatu baadae Cristiano Ronaldo akaifungia Real Madrid bao la pili na kukataa kushangilia.

Modric akifumua shuti lililozaa goli la kwanza

Ronaldo akinyanyua mikono kupinga kushangilia goli lake
Dakika
kumi za mwisho mpira uliweka kambi ya kudumu kwenye lango la Real
Madrid lakini kipa Lopez alikuwa mwiba kwa United kwa kufuta michomo
mingi.

Mambo yalipokuwa magumu kwa Ramos
Baada
ya mpira kumalizika Ronaldo aliyeichezea United kabla ya kujiunga
Madrid alitoka kichwa chini na kukwepa shamra shamra za wachezaji
wenzake huku mara chache akiinua macho yake yaliyoonyesha simanzi kwa
mashabiki wa United na kuwapungia.
Kocha
wa Real Madrid Jose Mourinho alipohojiwa kuhusu utata wa mwamuzi,
aliongea maneno machache na kuondoka: “Mbali na mwamuzi, timu bora
imetolewa, hatukucheza vizuri, hatukustahili kushinda”.
Katika mchezo wa kwanza uliofanyika Hispania timu hizo zilifungana 1-1.
MAN UNITED:
De Gea, Rafael, Vidic, Ferdinand, Evra, Carrick, Cleverley, Nani,
Welbeck, Giggs, Van Persie. Subs: Rooney (Cleverly 73), Young (Welbeck
80), Valencia (Rafael 87).
REAL MADRID: Diego
Lopez, Arbeloa, Varane, Sergio Ramos, Fabio Coentrao, Khedira, Alonso,
Di Maria, Ozil, Ronaldo, Higuain. Pepe (Ozil 71), Kaka (Di Maria 45),
Modric.
No comments:
Post a Comment