HOJA
ya Mbunge wa Ubungo, John Mnyika (CHADEMA) kuhusiana na suala la tatizo
la upatikanaji wa maji katika Mkoa wa Dar es Salaam, inaelekea kupata
ufumbuzi kutokana na Rais Jakaya Kikwete kumuita Ikulu mbunge huyo
Jumatatu wiki ijayo.
Wengine
walioitwa kukutana na rais ni Mkuu wa Mkoa, Mecky Sadick, wakuu wote wa
wilaya pamoja na wabunge na wataalamu kutoka Wizara ya Maji.
Akizungumza
jana jijini Dar es Salaam katika uzinduzi wa daraja la Mtaa wa Golani,
Kata ya Saranga, Rais Kikwete alisema kuwa kutokana na wananchi wa kata
hiyo kupiga kelele kuhusiana na suala la maji ameamua kukutana na
viongozi hao ili kupatiwa ufumbuzi.
Kikwete
pia alitaka kuwepo na mfumo maalumu wa mabomba ya maji yatakayojengwa
kwa saruji kutoka Ruvu Chini na kuja jijini Dar es Salaam moja kwa moja
bila kuchepuliwa sehemu yeyote.
Katika hatua nyingine, Rais Kikwete alikiri kuwepo kwa wizi wa maji katika maeneo ambayo mabomba ya maji yamepita.
“Watu
wasifanye ukanjanja katika masuala ya maji, mabomba yanatandazwa na
watu wanaiba maji, shida inayotokea ni maji hayo kutokufika jijini Dar
es Salaam,” alisema.
Alifafanua
kuwa lita milioni 65 zinahitajika ili kukabiliana na tatizo la maji na
kwamba upanuzi wa Ruvu Juu na Chini ujenzi wake utakamilika Julai na
kutaka hatua za haraka kuchukuliwa kuhakikisha maji yanapatikana kwa
haraka ili kumaliza tatizo.
Hatua
ya Mnyika kuitwa Ikulu imetokana na kusimama kidete katika suala la
maji ambapo Aprili 4, mwaka huu aliwasilisha hoja binafsi na kuitaka
serikali kuchukua hatua za haraka za kuboresha upatikanaji wa maji safi
na ushughulikiaji wa maji taka katika Jiji la Dar es Salaam hoja ambayo
ili iliondolewa bungeni kibabe.
No comments:
Post a Comment