EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Friday, March 8, 2013

Mwakyembe akumbana na madudu mengine bandarini

WAZIRI wa Uchukuzi, Dk Harisson Mwakyembe amekutana na malalamiko mazito  kutoka kwa Chama cha Wakala wa Forodha (TAFFA) ambao wamedai kuna wamiliki wa meli ambao pia wanafanya kazi ya kuingiza na kutoa mizigo bandarini jambo ambalo ni kinyume cha sheria.
Kwa mujibu wa sheria za Mamlaka ya Udhibiti wa Vyombo vya Usafiri wa Majini na Nchi Kavu (Sumatra) ni marufuku kampuni ya wakala wa meli kuwa na leseni ya kuingiza na kupakuwa mizigo bandarini.

Akizungumza mbele ya Waziri Mwakyembe ambaye alialikwa katika mkutano uliohusisha wadau wa kampuni za ushuru wa forodha, Makamu mwenyekiti mstaafu wa Taifa, Otieno Igogo alisema, Serikali imekosa macho ya kuona baadhi ya udanganyifu unaotumiwa na baadhi ya vigogo kupitia mamlaka za hapa nchini.

Waziri Mwakyembe alidai kushtushwa na tuhuma hizo na aliagiza apewe majina ya kampuni hizo haraka ili aweze kuchukua hatua dhidi yao.

“Hatuwezi kuonekana kama tuko likizo lazima mniletee ushahidi ofisini kwangu,” alisema.
kiongozi huyo mstaafu Taifa.  Alibainisha katika mkutano huo kuwa , kitendo cha umiliki wa leseni mbili kwa kampuni hizo kunaweza kuruhusu mazingira yanayoshawishi vitendo vya kifisadi kufanyika kwa urahisi.

“Kampuni ya kupakuwa mizigo halafu pia inahusika na uwakala wa kupokea mizigo ya nje ya nchi na kutoa ndani ya nchi, Mheshiwa Waziri tunaomba uangalie hilo kwani pia linaondoa ushindani wa kibiashara,”alisema Igogo.

Alizitaja baadhi ya kampuni hizo kuwa ni pamoja na Swizz Port na DHL huku akiitupia lawama mamlaka ya Sumatra kwa kushindwa kuzichukulia hatua kampuni hizo.

Igogo ambaye ni Mwenyekiti wa Chama cha Walipa Kodi nchini aliongeza kuwa kwa mujibu wa  sheria katika umiliki wa kampuni za uwakala wa meli,Mtanzania anatakiwa kuwa na asilimia 51 ya umiliki lakini mpaka  sasa  hakuna kampuni hata moja inayomiliki asilimia hizo.

“Mheshimiwa Waziri, Kampuni hizo wanamiliki kampuni za meli, Watanzania wameshikizwa kama kivuli tu”alisema Igogo.

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate