Imetokea leo hii Morogoro Road na
Indira Gandhi,inasemekana Watu wapatao 60
walikuwepo ndani yake.. watoto wa Madrassa walikuwemo katika jengo hili
na pia mpaka sasa maiti zilizoopolewa ni zaidi 60 na majeruhi zaidi ya 30
wamekimbizwa hospitali, Bado pia kuna baadhi ya watu hai ndani yake.
Jitihada za uokoaji zimeanza kufanyika, Waziri Nchimbi tayari
amekwishafika eneo la tukio mpaka sasa japo kuna uhaba wa vyombo
vinavyostahili kushughulikia hali hii.
Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Slaa, jengo lenye ghorofa zaidi ya 12 jijini Dar es Salaam limeanguka na kusababisha vifo vya makumi ya watu.
Inasadikika watoto waliokuwa wanacheza kwenye uwanja wa michezo na wafanyakazi wa ujenzi wamefukiwa. Kwa sasa tunaendelea na jitihada za uokozi na tutatoa taarifa baadae.”
BBC Swahili: Kulingana na walioshuhudia ajali hiyo, watu walisikika wakipiga mayowe kutaka msaada.
“nilidhani lilikuwa tetemeko la ardhi, na kisha nikasikia mayowe,” alisema shahidi mmoja.Jengo hilo liko katikati mwa Dar es Salaam na lilianguka saa tatu kasorobo asubuhi kwa saa za afrika mashariki. Mamia ya watu wanaaminika kuwa ndani ya jengo hilo huku wengine wakiwa nje wakati wa ajali hiyo . Hata hivyo idadi kamili ya watu hao bado haujulikani.
Nayo website ya Global Publisher imeandika: Taarifa zilizotufikia ni kwamba jengo lenye ghorofa 16 lililokuwa bado linaendelea kujengwa katika makutano ya barabara ya Indira Gandhi na Morogoro jirani na Burhani limeanguka. Inasemekana katika jengo hilo kulikuwa na watu takribani 60 ambao wanahofia kupoteza maisha.
No comments:
Post a Comment