Habari na saluti5
NYOTA
wa filamu, Rose Ndauka amemzungumzia msanii mwenzie wa filamu, Kajala
Masanja aliyeponea chupuchupu kwenda jela miaka mitano na kusema kuwa,
anachoamini ni kwamba sasa Kajala atajipanga na kuyafanya maisha yake
yaende kama alivyokusudia hatimaye kutimiza ndoto zake.
Saluti5
ilizungumza na Rose ili kupata maoni yake juu ya kuachiwa huru kwa
Kajala aliyekuwa jela kwa muda mrefu, ambapo alisema kuwa kikubwa ni
kushukuru mungu kwa kuweza kwake kurudi tena uraini, lakini pia sasa ni
wakati wa kuzijenga upya ndoto zake.
“Binafsi,
siwezi kujua kwa sasa Kajala mwenyewe amepanga kitu gani juu ya maisha
yake, lakini ninaamini atafanya yale anayayowaza katika akili yake,
hususan kuhusiana na kuendeleza mipango yake ya kimaisha,” alisema Rose.
No comments:
Post a Comment