Wakili anayemtetea Wilfred Lwakatare, Peter Kibatara (kulia), akimueleza jambo Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe.
Mbowe akiwaeleza wanahabari njama za serikali kutaka kukidhoofisha chama chake.
Wakili Kibatara akiwafafanulia jambo wanahabari.
Mbowe akimtuliza mke wa Lwakatare baada ya mumewe kushindwa kutoka kwa dhamana.Mbowe akiwaeleza wanahabari njama za serikali kutaka kukidhoofisha chama chake.
Wakili Kibatara akiwafafanulia jambo wanahabari.
Kikosi cha mbwa kikiwa tayari baada ya wafuasi wa Chadema kuanza kupiga mbiu za "Pipoooz.."
Mbwa wa polisi akiwaangalia wafuasi wa Chadema (hawapo pichani) kwa 'uchu'.
Askari magereza nao walikaa mkao wa kazi.
Kila mmoja akitawanyika kivyake baada ya mkwara wa polisi.
Jana asubuhi mbwa wa polisi waliwatuliza
wafuasi wa Chadema waliofika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar
kusikiliza kesi ya ugaidi inayomkabili Mkuu wa Kitengo cha Ulinzi na
Usalama wa Chama hicho, Wilfred Muganyizi Lwakatare. Polisi wa kikosi
cha mbwa na vikosi vingine walikaa tayari kuwadhibiti wafuasi hao
walioanza kupiga mbiu ya chama hicho ya "Pipooooz..." baada ya kiongozi
wao kushindwa kutolewa kwa dhamana. Lwakatare amerudishwa tena rumande
baada ya kufutiwa mashitaka yake yote yanayomkabili na baadaye kukamatwa
na kurudishwa rumande. Kesi yake itatajwa tena Aprili 3, mwaka huu.
(PICHA ZOTE NA RICHARD BUKOS / GPL)
(PICHA ZOTE NA RICHARD BUKOS / GPL)
No comments:
Post a Comment